Matiko nitaendelea kushirikiana na wanachi ili kujenga ofisi za Mitaa atoa mifuko 40 ya saruji mtaa wa Gimenya.

Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akikabidhi  mifuko 40 kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa  Gimenya kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mtaa ili kupunguzia wanachi kutembea umbali mrefu kufuata huduma maktika  ofisi ya kata.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Gimenya Saasita akishukuru Mbunge baada ya kupokea msaada wa mifuko hiyo

Mmoja wa wananchi akibeba mifuko hiyo




Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini kupitia chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa ataendelea kuunga juhudi za waanchi pamoja na viongozi katika kuhakikisha wanajenga ofisi za Mitaa ili kuwaondolea hadha wanayoipata wanachi kufuata huduma umbali mrefu likiwemo suala zima la huduma zinazotolewa majumbani .

 



“Nia yangu ni kutumia kile kidogo ninachokipata ili kuboresha utendaji kazi wa viongozi, kuboresha Elimu Afya, na Maji kama sera yangu ilivyokuwa inasema kipindi cha kampeni” alisema Matiko.

 



Mbunge huyo alitoa Mifuko 40 ya saruji  ili ujenzi wa ofisi ya Mtaa wa Gimenya ukaanze mara moja kwa lengo la kupunguza hadha wanayoipata wananchi wake.

Powered by Blogger.