MAPITIO YA MKATABA KATI YA TBC NA STRATIMES KUMALIZIKA MWEZI APRIL:WAZIRI NAPE




 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(aliyesimama) akizungumza na Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii pamoja na Uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati kamati hiyo chini ya mwenyekiti Mhe. Peter Serukamaba (Mb) ilipotembelea Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam .

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba(Mb) (aliyesimama)akitoa maelezo mafupi kuhusu dhumuni la ziara ya kamati hiyo katika  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) katika kikao kazi wakati kamati hiyo  ilipotembelea TBC  leo Jijini Dar es Salaam .Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.

Mkurugenzi wa Shirika la la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Ryioba(aliyesimama) akieleza utendaji kazi wa Shirika kwa Kamati ya Bunge ya maendeleo ya Jamii wakati kamati hiyo ilipotembelea TBC leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Kulia  ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu.

Picha zote  na Shamimu Nyaki.
Powered by Blogger.