BOSI WA CLOUDS MEDIA RUGE ATHIBITISHA MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA USIKU AKIWA NA ASKARI WENYE SILAHA

Leo Jumatatu Machi 20,2017 mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ametoa ufafanuzi kuhusu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media Group usiku akiwa na askari wenye silaha wakati wa kipindi cha Shirika la Wambea Duniani (SHILAWADU)

Ruge: Niliwambia SHILAWADU siku ya Alhamis mchana kuwa wasiirushe 'Story' bila kuongea na upande wa pili (wa Gwajima)

Ruge: Niliwambia Vijana wa SHILAWADU kuwa 'Story' kama ndiyo anayoisubiri RC basi ajue haitaenda hewani hata kwny Social Media.

Ruge: Ijumaa niliwasisitiza SHILAWADU kuwa kipindi kile kisirushwe kwa kuwa 'Story' haiko balanced.

Ruge: Ijumaa saa 5 kasoro usiku nilipigiwa simu kuwa RC Makonda alikuwa kaja ofisini akiwa na maaskari wakiwa na silaha.

Ruge: Nilimpigia simu RC Makonda kumhoji kwanini aje ofisini na maaskari wenye silaha? Akauliza kwanini nimezuia kipindi kuruka?

Ruge: RC Makonda alikata simu, lakini nilipaniki nikiwazia hizo silaha walizokuja nazo ofisini.

Ruge: Paul Makonda ambaye ni rafiki yetu ametukosea,huwezi kuja ofisini kwetu usiku na tena na mabunduki,Makonda ana namba zangu kwanini asinipigie,Paul alikuwa rafiki yetu tangu akiwa mkuu wa wilaya na mimi siwezi kukataa urafiki.

Ruge: Walipofika ofisini waliondoka na FLASH yenye kipindi.

Ruge: RC Makonda alisema "Bahati yenu" baada ya kujua kuwa waliokataa vijana wa SHILAWADU sio waliozuia kipindi isipokuwa mimi.

Ruge: Nilimwambia Mkurugenzi wa Clouds(Kusaga) kuwa RC alitukosea heshima; kulikuwa na haja gani aje na silaha na ni rafiki yetu?

Ruge: Ukweli hakuna aliyepigwa ila kulijengwa hofu kubwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media. Si jambo dogo hili!

Ruge: Tusikwepe ukweli kuwa sisi Clouds Media kama chombo cha habari tuna wajibu wa ku-balance story. Sijawahi kulazimishwa story.

Ruge: Makonda alitaka stori iruke wakati haijabalance,mimi kama msimamizi mkuu wa vipindi nilikataa.

Ruge: Kuacha shughuli za kazi, Makonda amekuwa akija hapa Clouds kama rafiki. Ila kitendo cha kuja na walinzi kiliwashtua walinzi.

Ruge: Kama watanzania, hatutaki kuiona bunduki mitaani. Hili limetokea kutufungua macho kujua ma-RC na ma-DC wanavyofanya kazi yao.

Ruge: Sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi wetu wasitiwe hofu. Mimi sikuwekwa ndani, nilienda Polisi kuripoti suala hili.

Ruge: Vijana wa Shilawadu wameomba likizo wapumzike hawako vizuri.

Ruge: Sisi Clouds Media tumeumia sana kwa haya aliyofanya Makonda,We want Respect,we want Heshima tu.

Ruge: Mtu akikosea kabla hatujaangalia cheo chake, tuangalie makosa yake. Si kudai eti wanaomkosoa wanapingana Vita ya Dawa za Kulevya

Ruge: Mtu kuwa na nafasi ya Uongozi flani si sababu ya 'kuwapanda' watu . All we want is RESPECT!

Ruge: Ishu imetokea Ijumaa niliamini Makonda atakuja kuomba radhi Jumamosi.

Ruge: Mimi namlaumu kwa kitendo alichofanya,kwanza alikua rafiki,kwanza ni mkuu wa mkoa,urafiki wa mtutu hauhitajiki.

Ruge: Video clips za CCTV zinazozunguka mtandaoni kweli ni za hapa Clouds Media. Sisi tulidhani Makonda angeomba radhi kwa kadhia hii

Ruge: Siujutii ukaribu wangu na Makonda. Hata akirudi akaomba radhi bado nitamfikiria! Tunataka kuendelea kumpa ushirikiano

Ruge: Niseme, urafiki na BUNDUKI siutaki. Wanaodai Makonda alikuja hapa Clouds akiwa rafiki wanapotosha!

Ruge: Ametumia vibaya madaraka yake

Ruge: Clouds inalaani kilichotokea, na inaomba vyombo vya Habari vitoe ushirikiano katika kukemea hili.

Ruge: Kikubwa hatutaki kutengeneza hali yoyote ya kuyumbisha serikali,hatutaki kugombana na serikali.

Powered by Blogger.