Baraza Kuu la
Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limekutana Jijini Dar es salaam kwa
ajiri ya kujadili na kufanya uteuzi wa majina ya wagombea wa bunge la
AfriKa Mashariki yatakaopelekwa kwa Katibu wa bunge ili kupigiwa kura
na bunge la Muungano wa Tanzania
Mwenyekiti wa
chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba, jana alisema baraza litafuata
taratibu zilizotolewa na Katibu wa bunge ambazo zinakitaka chama kuwa
wazi ikiwa ni pamoja na kupeleka maombi ofisini au kwa barua pepe.
Mbali na kuteua
wagombea wa Afrika Mashariki, baraza litajadili hali ya kisiasa Tanzania
bara na Tanzania Zanzibar ili kubaini dira ya chama hicho kwa wakati
huu, huku likipitisha wakurugenzi wa chama hicho na kuteua bodi mpya ya
wadhamini ya chama hicho kwani iliyopo imemaliza muda wake.
Imeandaliwa na James Salvatory, BMG Dar