Zari Asema Hawezi Kumpeleka Diamond mahakamani kwa Sababu ya Matunzo ya Watoto
Mwanamama
Zari the Bossy Lady ambae alibahatika kupata watoto wawili na msanii
Diamon Platinumz lakini baadae wawili hao walikuja kutengana hivyo Zari
kuondoka na watoto na kwenda nao afrika kusini amefunguka na kusema kuwa
hata siku moja hawezi na hajawahi kufikiria kwenda kumpeleka mwanaume
huyo mahakamani kwa sababu ya matunzo ya watoto.
Akiongea
na waandsihi wa habari nchi Kenya, Zari amesema kuwa anatengeneza pesa
zake mwenyewe ambazo zinamtosha kwa ajili ya matunzo yake na watoto wake
kwahiyo hawezi kuhangaika kumpeleka Diamond mahakamani kwa sababu hiyo
kama wanawake wengine.
Katika historia, Diamond alishawahi kupelekwa mahakamani na Hamisa Mobeto kutokana na kushindwa kutoa matunzo ya mtoto .
Zari
ambae ana watoto watano huku watatu wakiwa wa mwanaume mwingine ambae
pia alishafariki, amekuwa akionekana kuwalea watoto wake kwa starehe
bila shida yoyote kutokana na kusadikika kuwa mwanamke huyo ni tajiri na
hana shida ya kuomba misaada.