Wazee wa Mila wasioshiriki Mikutano ya kutoa Elimu ya Kupinga Ukeketaji...



Wazee
wa Mila Muungano wa Koo 12 wakiwa katika Mkutano wa hadhara Kijiji cha
Ng'ereng'ere kwa lengo la kutoa elimu ya Kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto
wa Kike.


Wazee hao wamedai kuwa suala la Kupinga Ukeketaji
kwa sasa wameungana pamoja koo12 zote hivyo baadhi ya wazee hao ambao
hawashiriki Mikutano hiyo endapo watashawishi kukeketa mtoto wa kike
wachukuliwe hatua kali kwani watakuwa wamekiuka Makubaliano yao.


"Sisi
wazee sasa tupo koo ya  Wakira lakini wazee Wengine ambao tumekuwa nao
kwenye vikao vyetu vya Muungano hawapo  kwenye Mkutano wetu je wanamaana
gani serikali tunaomba muchukue hatua kali endapo watabainika Kukeketa
na pia walipita kila Nyumba kugomesha watu wasifike kwenye Mkutano"
walisema Wazee hao.


               Wananchi wakiwa katika Mkutano huo.

Mwita Nyasibora mzee wa Mila Koo ya Butimbaru akitoa elimu kwa Wananchi kutoka Koo ya Wakira.

Wangubo Mtongori mzee wa Mila kutoka Koo ya Wakira akitoa Elimu ya kupinga ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.


Sinda
Nyangole Mwenyekiti wa wazee wa Mila Koo ya wakira akitoa elimu hiyo
katika Mkutano wa hadhara nakuomba kukutanisha wale wazee ambao
wamesusia kikao hicho.

Winfrida
Ezekiel Mwita  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Remagwe akitoa ushuhuda
baada ya kupinga Ukeketaji na kupatiwa Elimu kipindi Kambi okozi ya
Masanga ilipoanzishwa Mwaka 2008 na kwa sasa ni Kiongozi wa Mfano katika
Jamii.

Zawadi Temba Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyabichune akifafanua jambo ambapo amesisitiza suala la Elimu kwa Mtoto wa Kike.

Afisa
Mtendaji wa kata ya Regicheri Meshaki Osward akisisitiza jambo ambapo
amesema wao kama serikali watashirikiana vyema na wazee wa Mila hao
katika kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.


Sister
Stella Mgaya ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Tarime
ambao wanapinga Ukatili wa kijinsia Ukiwemo ukeketaji kwa Mtoto wa Kike
akitaja Madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa kike na kuwataka wazee
kusimamia tamko lao ili kuondoa ukeketaji wilaya ya Tarime.


,,,Tazama Video hapa Chini kupata habari kamili,,,,
Powered by Blogger.