Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike,ni kichocheo kikubwa katika Ongezeko la Uto...
Afisa
Mtendaji kata ya Susuni Wilayani Tarime Mkoani Mara Meremo Matiko
akiongea na jamii katika Mkutano wa hadhara ulioitishwa na wazee wa Mila
Muungano wa Koo12 kwa lengo la kutoa Elimu juu ya Madhara ya Ukeketaji
kwa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime.
Afisa Mtendaji huyo amesema
kuwa suaala la Ukeketaji ni chanzo cha Mimba za Utotoni pamoja na
Ongezeko la Utoro katika Shule za Msingi na Sekondari kwani watoto
wanapokeketwa kipindi cha tohara ushindwa kwenda shuleni huku wengine
wakiolewa kwa kutambua kuwa sasa wamekuwa watu wazima.
"Sasa
wazee kama mmeamua kusimama na kutangaza suala la kuacha ukeketaji kwa
Mtoto wa Kike sasa watoto wetu watatimiza ndoto zao kwa kumaliza elimu
ya Msingi na Sekondari" alisema Matiko.
Licha ya kuwepo Ongezeko
la Utoro Mashuleni Matiko amesema ndoa nyingi zimekuwa zikuvunjika kwa
sababu ya mabinti kuolewa wakiwa wadogo na kushindwa kutimiza Majukumu
ya familia.
Muungano
wa wazee wa Mila koo12 wakiwa katika Mkutano wa hadhara Koo ya Bunchari
kata ya Susuni kwa lengo la kutoa Elimu Juu ya Madhara ya Ukeketaji kwa
Mtoto wa Kike.
Sister
Stella Mgaya ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga ambao
wanapiga Vita Ukeketaji akiteta jambo na Mmoja wa wazee wa Mila Muungano
wa Koo12 Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Mmoja wa wazee wa Mila kutoka Koo ya Bwirege Mzee Ezron Tembo akitoa elimu kwa Wananchi hao.
Badhi
ya Viongozi wa Serikali za Vijiji wakichangia katika Mkutano huo huku
wakipinga suala la kupaka Unga kwa Mtoto wa Kike kwa lengo la kutimiza
mila badala ya kukeketwa kulingana na madai ya wazee hao wa Mila.
Baadhi ya Wananchi wakichangia hoja katika Mkutano huo.
Sister
Stella Mgaya ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga akitoa
Elimu hiyo kwa Wananchi ambapo amesema kuwa sasa jamii itumikie Mwenyezi
Mungu huku wakilea watoto wao katika Maadili Mema.
Sister
ameongeza kuwa kwa kuwa tayari wazee wametangaza kuwa kwa mwaka huu
hakuna ukeketaji hivyo jamii kwa ujumla iungane kwa pamoja na kupinga
vikali suala la ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
,,,Tazama Video hapa Chini kupata habari Kamili,,,,