Makonda Kuwachukulia Hatua Kali Viongozi wa Michezo
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema atachukua hatua kwa
viongozi wa michezo ambao hawajafanya marekebisho ya uwanja wa Taifa wa
ndani 'indoor' licha ya kuwakabidhi pesa na vifaa mwaka jana.
Makonda
amesema Mei 18, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza
kuwa alikubali kujinyima na familia yake ikae gizani kwa kutoa jenereta
la nyumbani kwake ili kutimiza ahadi ambayo aliwahidi wanamichezo hao
lakini imekuwa kinyume na mategemeo.
“Lile
jenereta nililihamisha badala ya kuwepo nyumbani kwa mkuu wa mkoa
nikalikabidhi mwaka jana, sasa kama mpaka leo hii halijaenda basi
kutakuwa kuna shida mahala, na niwaambie tu siwezi kuahidi kitu
nisifanye hata kama ni cha kwangu nitajinyima, nimeinyima familia yangu
wakae gizani ili nihakikishe kwamba jenereta linakwenda kwa wapenzi wa
mpira” amesema Makonda.
Makonda
ameongeza kuwa atawasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es salaam, Lazaro Mambosasa ili aweze kuwachukulia hatua watu ambao
wameshibdwa kutimiza majukumu yao
Mkuu
wa Mkoa Makonda amesema mwaka jana alikabidhi pesa, mipira, mabati na
jenereta ili kusaidia uwanja wa Taifa wa ndani uliokuwa katika hali
mbaya na hivyo anashangaa kusikia bado hakuna kilichofanyika mpaka sasa.