Makamba azindua mwongozo wa tathmini ya athari za mazingira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January
Makamba amezindua Muongozo wa Tathmini ya Mazingira (SEA) ikiwa ni
sehemu ya juhudi za Serikali kulinda mazingira ili yaweze kuchochea
ukuaji wa uchumi na kuleta maendeleo endelevu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
“Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira,” Alisisitiza Mhe. Makamba.
Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara, Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda.