Kondakta Atiwa mbaroni kwa kukutwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia kondakta wa kampuni moja ya
mabasi yanayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya,baada ya
kumkuta na vipodozi vilivyopigwa marufuku.
Mtuhumiwa
huyo mkazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam alikutwa akiwa amehifadhi
vipodozi hivyo katika mifuko miwili ya plasitiki na kwenye boksi.
Akizungumza
leo Jumatano Mei 16, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich
Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya polisi kusimamisha basi
na kulifanyia upekuzi.
Amesema tukio hilo limetokea Mei 15, 2018 saa mbili usiku huko maeneo ya Melela Barabara Kuu ya Iringa-Morogoro.
Matei
amesema mtuhumiwa alikutwa na vipodozi katoni 56 vya aina tofauti na
kwamba vipodozi hivyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
Alivitaja
vipondozi hiyo kuwa ni Extra Claire tube katoni 23,Lemon Vert Cream
katoni 12, perfect white cream 6, betason 4, carolite 3, beiaton 2,
extra cream1, sivop cream 1, dyna Claire 1, lemonvet cream 1, princes
tube cream 1, epiderm cream 1, exoplus boksi 1, actilua lotion dazen 11,
demon Claire pakti 3, oranvet jelly pakti 3 na Claire for men 11
Katika
tukio lingine kamanda Matei amesema polisi wanamshikilia mkazi wa
Kikwalaza tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa kwa tuhuma za kukutwa na meno
ya tembo yenye uzito wa kilogramu 10 zenye thamani ya Sh34 milioni ,
akiwa amezipakia kwenye baiskeli.
Kamanda Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 15, 2018 na polisi wakishilikiana na maofisa wanyamapori.
Amesema alikutwa akiwa amepakia meno hayo katika baiskeli.
