DC SHINYANGA AZINDUA RASMI ZOEZI LA KUGAWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro amezindua rasmi zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa
(NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Mei 16,2018 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi
vitambulisho 12,918 kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa hiyo
watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
“Hapa nchini, hili ni zoezi la kwanza la
ugawaji vitambulisho kwa wananchi kwa kutumia ugawaji wa
mkupuo,tunaanzia katika manispaa ya Shinyanga,nakabidhi rasmi
vitambulisho hivi kwa maafisa watendaji wa kata ambao watagawa
vitambulisho kwa wananchi”,alieleza Matiro.
Aidha aliwataka maafisa watendaji kuwa
makini na kugawa vitambulisho hivyo haraka huku akisisitiza kuwa
vitambulisho hivyo havitolewi kwa ubaguzi bali kila mwananchi ana haki
ya kupata.
“Zoezi kujiandikisha linaendelea katika
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lakini kwa upande wa manispaa ya
Shinyanga tumemaliza zoezi la uandikishaji kinachoendelea sasa ni kugawa
vitambulisho,hili ni zoezi endelevu wale ambao hawajiandikisha wafike
katika ofisi za NIDA kujiandikisha ili wapate vitambulisho”,aliongeza
Matiro.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
huo,Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau alisema
tangu waanze zoezi la uandikishaji mwezi Septemba 2017 katika manispaa
ya Shinyanga wamezalisha jumla ya vitambulisho 17,780 na tayari
wameshagawa vitambulisho 3651 kwa watumishi wa umma na leo vitambulisho
12,918 kwa wananchi na zoezi la uandikishaji na ugawaji vitambulisho
linaendelea.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa
Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa aliwasisitiza wananchi ambao
bado hawajisajili waendelee kujisajili katika ofisi za Uhamiaji huku
akiwataka kutoa ushirikiano kuwafichua watu wasiostahili kupata
vitambulisho hivyo.
“Uzalishaji wa vitambulisho unaendelea
na tunatarajia hadi mwezi Desemba mwaka huu kila mwanachi awe na
kitambulisho,NIDA inaomba wananchi kufichua watu wasiotahili kupata
vitambulisho hivi wakiwemo wahamiaji haramu”,aliongeza Kapesa.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi aliwataka maafisa watendaji
kutoendekeza urasimu katika ugawaji wa vitambulisho na hatarajii kusikia
kitambulisho cha mwananchi kimepotea.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa
vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,
Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa
vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akiwasisitiza maafisa watendaji wa kata kuwa makini
katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wananchi ili kuepuka changamoto
inayoweza kujitokeza ya kupotea kwa vitambulisho.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga
Nathanael Fredrick Njau akisoma taarifa ya zoezi la uandikishaji na
utoaji vitambulisho vya taifa katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa
Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa akizungumzia kuhusu zoezi la
utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi
la ugawaji vitambulisho.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga, Agnes Machiya akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro kuzindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya
taifa kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya vitambulisho 12,918
vilivyokabidhiwa kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa ya
Shinyanga watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa Naibu Meya wa
Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya wakati akizindua rasmi zoezi la
kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akionesha kitambulisho chake cha taifa
baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa diwani wa kata ya
Lubaga Mchungaji Obedi Jilala (CHADEMA).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa diwani wa viti
Maalum Manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka (CCM).
Diwani wa kata ya Kizumbi,Reuben Kitinya akipokea kitambulisho cha taifa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akikabidhi Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji
wa kata ya Mwawaza,Nhiga Nhiga ili akavigawe kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa
Josephine Matiro akikabidhi Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji
wa kata ya Ndembezi,Felister Msemelwa ili akavigawe kwa wananchi wa kata
hiyo.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga
Nathanael Fredrick Njau akisisitiza jambo wakati wa zoezi la ugawaji
vitambulisho vya taifa kwa maafisa watendaji wa kata za manispaa ya
Shinyanga.
Maafisa watendaji na madiwani wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog