Baba Atiwa Mbaroni Kwa Kumuua Mwanae Kwa Kichapo
Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauji dhidi ya mtoto wake wilayani ukerewe.
Mnamo
tarehe 23.05.2018 majira ya saa 14:00hrs mchana katika kijiji cha
Hamkoko kilichopo wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza, mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Buyanza Magayane miaka 39, mkulima na mkazi wa
kijiji cha Hamkoko, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za
mauaji ya mtoto wake wa kumzaa aitwaye Baraka Buyanza, miaka 02, hii ni
baada ya kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na
marehemu kujisaidia kinyesi kwenye maeneo mbalimbali ya nyumba hali
iliyopelekea marehemu kupoteza maisha kisha kumzika katika shamba lake
lililopo nyuma ya nyumba yake, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Awali
inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ametengana na mkewe yani mama wa
marehemu kwa muda mrefu, hivyo marehemu alikua akiisha na baba yake
mzazi anayetuhumiwa kusababisha kifo chake pamoja na mama yake wa
kambo.
Inasemekana
kuwa tarehe tajwa hapo juu mtuhumiwa alikuwa ametoka kwenye shughuli
zake za kila siku ndipo aliporudi nyumbani alimkuta marehemu akiwa
amejisaidia kinyesi katika sehemu tofautitofauti za nyumba yake ndipo
alimchukua kisha kumchapa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kisha
alimfungia ndani ya chumba peke yake.
Inadaiwa
kuwa baada ya muda kupita mtuhumiwa alikwenda kumuangalia mtoto
chumbani alipokuwa amemfungia, ndipo alikuta tayari mtoto amefariki
dunia.
Inasemekana
kuwa baada ya kuona hali hiyo mtuhumiwa alikwenda kuchimba shimo katika
shamba lake lililopo nyuma ya nyumba yake kisha alimzika mtoto, lakini
majirani waliona kitendo kile kisha walitoa taarifa kituo cha polisi
ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na
kufanikiwa kumakamata mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye alikiri kufanya
mauaji hayo na kuwapeleka askari sehemu alipomzika marehemu.
Mwili
wa marehemu tayari umefukuliwa, umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya
ya ukerewe kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika
utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Polisi
wapo katika mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze
kuchukuliwa dhidi yake
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa
wito kwa walezi na wazazi akiwataka kuacha tabia ya kutoa adhabu za
vipigo mara kwa mara kwa watoto pindi wanapokosea bali wawaelekeze kwa
hekima na busara na kuwafundisha ili kuepusha majeruhi,ulemavu na vifo
vya aina kama hii ambavyo vitapeleka mzazi kufungwa.