Waziri Nchemba amwagiza IGP kufanya uchunguzi wa mauaji ya kiongozi wa Chadema
Waziri
wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la
Polisi IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya
mauaji ya Daniel John ambaye alikuwa ni Katibu wa kata ya Hananasifu
(Chadema) yaliyotokea Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Waziri
Mwigulu amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na
kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
“Mataifa
mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya
watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida
tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,”
alisema Waziri Mwigulu.
Ameongeza kusema kuwa maswala ya demokrasia huamukiwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki.
