WATENDAJI TIMIZENI WAJIBU WENU KUONDOA MIGOGORO – IYOMBE
|
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, aliyepo katikati Mhandisi Mussa Iyombe akisomewa
taarifa ya mkoa wa Manyara na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Misaile
Mussa ofisini kwake Babati Manyara
|
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe akiongea na watumishi wa
Halmashauri ya Babati na Babati Mji katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya
Babati wakati wa ziara yake
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI)
walioshiriki ziara ya Katibu Mkuu OR TAMISEMI Mha. Mussa Iyombe wakiwa katika chumba cha mikutano Babati.
Katika
picha ya pamoja ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe na
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Misaile Mussa wakisikiliza taarifa ya
Halmashauri ya Mji Babati.
Baadhi
ya watumishi wa ofisi ya Mkoa wa Manyara, Babati Mji na Halmashauri ya Wilaya
Babati wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe
alipokuwa akiongea nao mjini Babati.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe alipowasili katika ukumbi
wa Halmashauri ya Wilaya Babati kuongea
na watumishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe amewaasa watendajii wa mkoa wa Manyara kuchukua
hatua stahiki zinazohusu masuala ya watumishi ili kupunguza au kuondoa migogoro
mkoani Manyara.
Katibu Mkuu Mhandisi
Iyombe ameyasema hayo mjini Babati wakati akiongea na watendaji na watumishi wa
Mkoa wa Manyara, Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya Babati
kwamba kiwango kikubwa cha migogoro hasa ya ardhi mkoani humo inatokana na
baadhi ya watendaji kutotimiza wajibu wao ipasavyo hali wakizingatia sheria na
taratibu za nchi.
“migogoro mingi inaanzia
Sight (sehemu wanazotwaa ardhi ili kupima) kwa kuleta taarifa iliyo na
mapungufu na pia zingatieni sheria za ardhi, migogoro ipungue kwa kwa kutenda”
Pia Mhandisi Iyombe amesema
wapo Watendaji ambao wanashindwa kutumia Mamlaka waliyopewa na kuzuia migogoro
ya ardhi ambayo inazuilika lakini pia amehoji mbona mipaka ya mikoa na wilaya
ipo wazi na kwanini sehemu nyingine za kiutawala, “msilazimishe migogoro ya
ardhi kwani tumewapa mamlaka kwa kufanya Ugatuaji wa madaraka (D by D) hivyo
amueni”
Akipokea taarifa ya elimu
kuhusu kuwashusha vyeo walimu wakuu zaidi ya 250, ametoa angalizo kuwa mamlaka
na Uongozi wa mkoa mzima unapaswa kushauriana katika masuala mbalimbali kama
hilo la elimu kabla ya kuchukua maamuzi magumu ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina
kwani yanaleta athari kiutendaji na kisaikolojia kwa watumishi.
Mhandisi Iyombe amewataka
watendaji wa mkoa kuepuka suala la kuwa na Maafisa wengi wanaokaimu hali sheria
zipo wazi kwani kufanya hivyo kunapunguza hamasa ya utendaji na kuongeza
gharama zisizo za lazima. “suala la kukaimu lisizidi miezi sita ili kuboresha
utendaji, kwanini Halmashauri zingine wanakaimu hadi miaka mitatu” amewataka
kufuata sheria za kazi ili kupunguza hoja zisizo na msingi.
Kwa upande wake Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa Misaile Mussa amesema mkoa wa manyara una upungufu wa watumishi
wapatao 6644 kwa mkoa mzima ambapo watumishi 2,076 wapo Halmashauri ya wilaya
ya Babati. Lakini pia mkoa unakabiliwa na Maafisa wengi wanaokaimu kuanzia
ngazi ya mkoa na Halmashauri za mkoa huo.
Naye Mkuu wa wilaya ya
Babati, Mhe.Raymond Mushi amesema kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji na
hasa ya miundombinu ya kupeleka maji na pia mipaka ya wilaya ya Babati na
Monduli, na Babati na Kondoa anaendelea kufuatilia kuona mipaka halisi mahali
ilipo.
Katibu Mkuu Mhandisi Mussa
Iyombe yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Manyara ambapo leo hii
ameongea na watumishi hali akisikiliza kero zao na kuzitolea majibu papo hapo
na kesho atatembelea miradi ya maendeleo kujionea jinsi inavyotekelezwa.