Shirika la CDF Tarime Waadhimisha siku ya kupinga Ukeketaji Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiongea katika Maadhimisho ya Siku ya kupinga Ukeketaji duniani ambapo shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF limeadhimisha maadhimisho hayo katika shule ya Msingi Borega B huku viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini wakipiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji kwa Mtoto wa Kike. |
Wanafunzi wakiwa katika Maadhimisho hayo. |
Kambibi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akiongea katika Maadhimisho hayo ambapo ameeleza mikakati ya Shirika hilo na yale waliofanya kwa lengo la kutokomeza ukeketaji huku wakiunda Klabu mbalimbali ndani ya Shule na Nje ya shule na kutoa Elimu ya Ujasiriamali ili wahanga wa ukatili waweze kujishughulisha na kupata kipato huku wakiwa mabalozi wa kupinga na kutoa elimu juu ya madhara ya Ukeketaji. |
Mchungaji Oluochi akip[iga vita ukeketaji. |
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Borega B wakiimba nyimbo zenye ujumbe wa kuinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike. |
Kambibi Kamugisha kutoka CDF akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga katika Maadhimisho hayo. |
Samwel Metane kutoka AMREF/LHRC Serengeti akitoa takwimu za ukeketaji ambapo ametaji mikoa Mitano inayoongoza kwa ukeketaji hapa Nchini Ukiwemo Mkoa wa Mara ambapo unaongoza kwa Asilimia 32 huku Wilaya ya Tarime na Serengeti vikiongoza kwa ukeketaji. |
Tazama Video hapa Chini ili kupata habari kamili kuhusu Maadhimisho hayo. |