Michael Kembaki aliyegombea Ubunge Tarime Mjini CCM achangia ujenzi wa Z...
| Aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM 2015 Michael Kembaki akikabidhi fedha kwa Mhasibu wa Mtaa wa Masurura Kata ya Nyandoto Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mtaa huo ili kuokoa Maisha ya akina mama wanaotemmbea umbali zaidi ya Kilometa 14 kwenda na Kurudi kwa ajili ya kufuata huduma ya Afya Mjini Tarime. |
na Kembaki wananchi wa Mtaa huo wamedai kuwa Miundombinu ya Elimu, Afya
na Barabara kwao ni changamoto kubwa hivyo endapo Zahanati hiyo
itakamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa.
Kembaki
ameongeza kuwa katika kipindi cha kampeni 2015 alitoa ahadi ya
kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha Afya japo kura hazikutosha lakini
hawezi kukata tamaa katika kuchangia suala zima la Maendeleo ili kuokoa
maisha ya akina mama wanatembea umbali mrefu kufuata huduma ya Afya
ikiwa ni moja ya kuunga Juhudi za kuwalelea Wanachi Maendeleo
zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli.
Hivyo
Kembaki ametoa Mifuko 30 ya Saruji, ,Mawe ya kuanzia ujenzi pamoja na
Nondo 10 katika Ujenzi wa Vyumba Viwili vya Madarasa shule ya Msungi
Nyandoto.
| Kembaki akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya mtaa wa Masurura Kata ya Nyandoto Halmashauri ya Mji wa TarimeMkoani Mara. |
| Viongozi wa Mtaa wa Masurura Wakiangalia Ujenzi wa Vyumba viwilli vya Madarasa shule ya Msingi Nyandoto ambapo Kembaki ametoa Nondo 10 kwa ajili ya kuunga Mkono Nguvu za Wananchi hao. |
| Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyandoto akionyesha Nguvu za Wananchi katika Ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa shuleni hapo. |
| Wananchi wakielekea eneo la kujenga Zahanati ya Mtaa wa Masurura Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara. |
| Kushoto ni Diwani wa kata ya Nyandoto Fredy Sabega akieleza Michael Kembaki Mikakati aliyonayo katika ujenzi wa Zahanati ya Mtaa huo. |
| Kembaki akiongea na wananchi wa Mtaa wa Masurura. |
| Mwenyekiti wa Mtaa wa Masurura Marwa Jackson akitoa Shukrani zake kwa Kembaki huku akiwaomba wadau wote wa Maendelea kuwaunga Mkono katika Ujenzi wa Zahanati. |
| Diwani wa Kata ya Nyandoto Fredy Sabega akitoa Shukrani kwa niaba ya wananchi wake |