Makubwa haya !! ATUPWA JELA KWA KUMTILIA MKEWE PILIPILI KWENYE CHUPI....SEHEMU ZA SIRI ZIKAVIMBA
Mtu mmoja anyejulikana kwa jina la Moses
Okello amehukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi za jamii kwa siku
40, baada ya kukutwa na hatia ya kumtilia pilipili mke wake kwenye nguo
ya ndani 'chupi'.
Mke wa Okello aliiambia mahakama kuwa
mume wake huwa anapenda akiwa amevaa nguo hiyo, na siku hiyo
alimlazimisha sana kuivaa na kutekeleza, na baada ya muda mfupi alihisi
kuwashwa na kuvimba sehemu za siri na kuamua kwenda kumuona daktari,
ndipo walipogundua ilikuwa ni pilipili.
“Aliniambia anavutiwa sana na mimi
nikiwa nimevaa hiyo nguo akawa ananilazimisha kuivaa, baada ya kuivaa
nikaanza kuhisi muwasho sana, nikaenda kumuona daktari na kugundua
ilikuwa pilipili”, amesema Mke wa bwana Okello ambaye jina lake
limehifadhiwa.
Moses alikiri kufanya tukio hilo kwa mkewe, na kusema kwamba ulikuwa ni utani ambao amezoea kufanyiana na mke wake huyo kipenzi.