JAFO AAGIZA TATHMINI YA KINA IFANYIKE KUKAMILISHA JENGO LA HALMASHAURI YA CHAMWINO.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo
la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la
Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya
Chamwino Vumilia Nyamonga wakati akitoa maelezo kuhusu eneo lililotengwa kwa
ajili ya uboreshaji Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kujionea eneo
litakalotumika kuongeza majengo ya Kituo cha Afya Chamwino.
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kuagiza Wakala wa
Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya jengo hilo liweze
kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.
Watumishi
wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na
jengo lao kutokamilika.
Jafo
ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa
mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari
mosi mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa
zilizofanya kukwama kukamilishwa kwa jengo hilo.
“Jengo
hili awali lilikuwa linajengwa na mkandarasi mwingine lakini kutokana na
utendaji wake kutoridhisha tuliamua kumpatia Suma JKT na niliagiza jengo
likamilike Januari mosi mwaka huu, lakini bado halijakamilika,”alisema
Amesema
sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi
wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika
kwenye ubora unaotakiwa.
Waziri
Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na kwamba kwa kuwa wanaelekea katika
mipango ya bajeti wataangalia namna ya kushirikiana na Halmashauri ili jengo
liweze kukamilika.
Awali,
Mkandarasi kutoka Suma JKT, Mhandisi David Pallangyo amesema ukamilishaji
umekwamishwa kutokana na hali ya hewa na pia makosa yaliyofanywa na mkandarasi
wa awali.
“Hapa
hii flow ya chini tuliona tuikamilishe lakini hali ya hewa na hizi mvua maji
yanajaa hivyo tunafanya tathmini kama tutaweza ni vyema tukaweka water
proof,”amesema.
Aidha
Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Mhandisi Vilumba Sanga amesema wanafanya
tathmini katika jengo hilo kuangalia namna ya kulikamilisha kwa kushirikiana na
Suma JKT.
“Tunafanya
‘estimate’ ya water proof maana maji yanajaa, hii inatokana na makosa
yaliyofanywa na mkandarasi wa awali, huyu mkandarasi wa sasa anakutana nayo
site,”amesema Sanga
Katika
hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo Cha Afya cha Chamwino Ikulu
kuangalia uboreshaji wa kituo hicho ambacho kimeingiziwa Sh.Milioni 500 kwa
ajili ya kujenga Wodi ya akina mama na watoto, maabara, Chumba cha Kuhifadhia
maiti.
Hata
hivyo, amekuta ujenzi huo haujaanza kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa kuwa
dogo na hivyo kuahidi kufanya tathmini halisi kwa kushirikiana na wataalam
kuangalia uwezekano wa kujengwa jengo la ghorofa.