Waziri Nchemba aagiza vijana sita kuajiriwa na Serikali
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza vijana sita
ambao wanafanyakazi ya kujitolea katika mradi wa kiwanda cha sukari cha
Mbigiri wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro majina yao yapelekwe wizarani
wapate ajira ya kudumu.
Hatua
hiyo imefikia baada ya waziri Mwigulu kufika kiwandani hapo na kupata
taarifa ya kinachoendelea kiwandani hapo na kuambiwa kuwa kuna vijana
sita wenye taaluma mbalimbali ambao wanajitolea na wamefanya kazi kubwa
ya ujenzi wa kiwanda hicho na wengine kuchora ramani ya baadhi ya
majengo yenye umbo la ndege aina boeing.
“Msimamizi
wa mradi chukua majina ya hawa vijana yalete wizarani, tutayapeleka
utumishi ili hawa vijana wazalendo wawe ndio wafanyakazi wa kwanza wa
kiwanda hichi kwani kujitolea kwa miezi sita bila kulipwa tena kijijini
ni uzalendo wa hali ya juu na wanaipenda nchi yao,” alisema
Waziri
Nchemba amepongeza hatua iliyofikiwa mpaka sasa katika mradi huo kwani
sehemu kubwa ya miwa iliyopo shambani imekua mikubwa na kwa taarifa
alizopewa ifikapo mwezi wa nane mwaka huu wataanza kuvuna miwa na sukari
ya kwanza kutoka kiwandani hapo itatoka oktoba mwaka huu.
Naye
Msimamizi wa mradi wa kiwanda cha sukari Mbigiri Eng Robert Kabudi
amesema kwasasa wanaingia makubaliano na kampuni moja kwa ajili ya
ujenzi wa kiwanda cha sukari na kuleta mitambo ambapo kwa makadilio
ifikapo mwezi wanane kiwanda kitakua kimekamilika na kuanza uzalishaji
wa sukari.
“Mvua
kutokunyesha ya kutosha imekua changamoto kwetu hasa katika kupanda
miwa mingi zaidi kwa ekari zilizobaki lakini tunaendelea kuchimba visima
vingi zaidi kwa ajili ya umwagiliaji shambani na tunaendela vizuri
mpaka sasa kama unavyojionea na ifikapo mwezi wa nane mwaka huu tutaanza
kuvuna awamu ya kwanzu mheshimiwa,” alisema
Eng
Robert ameongeza kuwa mpaka sasa wameongezewa ekari 200 na wilaya ya
kilosa ambapo wanampango wa kujenga shule, kituo cha polisi na malls na
mabenki ilikufanya kijiji cha mbigiri kuwa cha kisasa kama kilombero na
sehemu zingine za viwanda ili wafanyakazi baadae wasifate huduma mbali.
Kiwanda
cha sukari cha mbigiri ni cha ubia kati ya jeshi la magereza nchini na
mifuko ya kijamii ya NSSF NA PPF na kinatarajiwa kuanza kutumika mwezi
october mwaka huu na uzalishaji wake utakua ni zaidi ya tani 30000 za
sukari kwa mwaka.