Kigwangalla aagiza polisi kuwakamata vigogo wanne, la sivyo atafikisha taarifa kwa Rais Magufuli
Waziri
wa Maliasili na utalii Dkt.Hamis Kigwangala amelitaka Jeshi la Polisi
kuhakikisha linawakamata watu wanne waliopanga mauaji ya mhamasishaji wa
utalii Wayne Lotter mwaka Jana jijini Dar es Salaam la sivyo atafikisha
taarifa hiyo kwa Rais John Magufuli.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa watu hao waliopanga kufanyika mauaji hayo ni vigogo wapo wanne na wanajulikana.
"Ninawajua
viongozi wanne ambao ni vigogo kuwa wameshiriki katika kupanga mauaji
ya mhamasishaji wa utalii nchini Wayne Lotter," alisema Dkt Kigwangalla
Kauli
hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo
Januari 25, 2018 na kusisitiza kuwa katika kipindi cha siku 100, wizara
yake imebaini mitandao 74 ya watu wanaojihusisha na ujangili ikiwa na
washiriki 949.
Amesema
kati ya watu hao, 949 tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka
yanayowakabili huku wengine wakisubiri kufikishwa mahakamani.