Auwa familia kwa wivu wa mapenzi
Mwanaume
mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa
Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana
na wivu wa mapenzi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo
usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha
kutokomea kusikojulikana.
“Ni
kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali
ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua
mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo
mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na
anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa
jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika.
Kamanda
Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo
marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiye
kafanya mauaji.
Jeshi
la Polisis limesema taarifa za tukio hilo walizipata kutoka kwa
majirani baada ya kugundua hakuna dalili ya kuwepo watu kwenye hiyo
nyumba na kuanza kuchunguza, ndipo walipogundua hayo na kuita polisi
kuvuja mlango.
Waliouawa
kwenye tukio hilo wametajwa kuwa ni Upendo Lukule ambaye ndiye mke,
Magreth Samuel ambaye ni shemeji mtu na mtoto mdogo ambaye umri wake ni
chini ya mwaka mmoja.