Mwigulu: Lazima Tubadili Sheria kuwabana zaidi
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema wizara yake
itahakikisha inawabana ipasavyo wahamiaji haramu pamoja na kubadilisha
sheria ili ziwabane zaidi.
Waziri
Mwigulu ameyasema hayo alipotembelea Gereza la Kigongoni wilayani
Bagamoyo na kugundua robo tatu ya wafungwa ni wahamiaji kutoka nchi
jirani ikiwemo Ethiopia.
Taarifa
ya Mkuu wa magereza Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, SACP Boyd Mwambingu imebainisha kuwa wafungwa ambao ni raia wa
Ethiopia waliofungwa katika Magereza ya Mkoa huo ni 334, Mahabusu 12 na
wanaosubiri kusafirishwa ni 91 ambao jumla ya raia kutoka Etheopia ni
437 wa Malawi ni 1 Msomali ni 1 wa DRC ni 1 wa Burundi 2 na Kenya ni 2.
Kufuatia
taarifa hiyo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema
haiwezekani wahamiaji haramu wagharamikiwe na taifa ikiwemo kusafirishwa
kwa gharama za serikali pamoja na kupatiwa Chakula na Matibabu.
“Tutafanyia
kazi ili sheria iseme kama watakamatwa watafungwa au mambo mawili, nchi
yao iwachukue au warudi kwa gharama zao wenyewe lakini sheria lazima
iwe kali itakayotoa fundisho kwa wengine”, amesema Mwigulu.