Makamu wa Rais wa Tanzania Mh Samia wanawake weka nguvu ya pamoja kupig...









Makamu wa rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Septemba 5,2017 amezindua tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017 lilirotaribiwa na TGNP Mtandao na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI).



















Tamasha hilo la siku nne linafanyika kuanzia Septemba 5 hadi 8,2017

katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam huku mada

kuu ikiwa ni “ Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa wa Kijinsia na

Maendeleo Endelevu”.







Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mheshimiwa Samia Suluhu alisema

serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa uzingatiaji wa masuala ya

jinsia katika kuchangia kuharakisha maendeleo ya nchi.





“Serikali kwa kushirikiana na na wadau mbalimbali tumechukua hatua za

maksudi ili kuhakikisha tunajenga jamii yenye usawa wa kijinsia na

uwezeshaji wa wanawake kama ilivyoainishwa katika mikataba na maazimio

mbalimbali ya kimataifa”,alieleza Suluhu.







Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi,kusimamia

utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuhakikisha wanawake na wanaume

wanashiriki kwa usawa katika kujiletea maendeleo pamoja na kunufaika na

maendeleo hayo.







Mheshimiwa Suluhu alitumia fursa hiyo kuwaasa wanawake

kupendana,kunyanyuana,kufahamishana na kuelimishana na kupigania haki

zao kwa kuzingatia mila na desturi zao.







Aidha aliipongeza TGNP kwa harakati zake za kuiunga mkono na kuikosoa serikali pale wanapoona imekwenda tofauti. 







Alisema kitendo cha kukemea na kutoa mapendekezo na suluhisho sehemu

ambayo wanaamini serikali haijafanya vizuri ni kitendo cha kiungwana na

kinachochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.







Aidha alizipongeza halmashauri za wilaya zinatoa asilimia 5 ya wanawake

huku akiwataka wazazi kutumia fursa ya elimu bure kupeleka watoto wao

shule ambapo takwimu zinaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa la watoto wa

kike waliopelekwa shule mwaka huu.







Mbali na uzinduzi huo ameongoza zoezi la kutoa tuzo kwa baadhi ya

akinamama waliofanya vizuri na kutoa mchango katika maendeleo ya

wanawake.







Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi

alisema Tamasha la Jinsia ni Jukwaa la wazi la wanawake na wadau wa haki

za binadamu ambalo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja likiratibiwa na

TGNP Mtandao lengo likiwa ni kushirikishana mafanikio,uzoefu,kuainisha

changamoto na kuweka mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo.







Alisema Tamasha hilo linalofanyika kila mara baada ya miaka miwili

linaandaliwa na taasisi kadhaa zinazotetea haki na usawa wa jinsia

zikiongozwa na TGNP Mtandao na mwaka huu limeshirikisha wanawake zaidi

ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.







Aliongeza kuwa tamasha hilo linajikita katika kutambua mchango wa

wanawake ambao wamekuwa mfano katika kuchochea maendeleo katika ngazi ya

kitaifa na kimataifa lakini pia wanaume ambao wamekuwa mfano katika

kutetea ajenda ya haki za wanawake.





“Malengo ya Tamasha hili ni kutafakari na kusherekea

mafanikio,kujadili changamoto na kuweka mikakati ya pamoja kutatua

changamoto hizo,kutathmini ushiriki wa wanawake katika michakato ya

kufanya maamuzi na katika ngazi ya uongozi",alifafanua.





"Malengo mengine ni kufuatilia,kuhifadhi, kutambua na kusherekea

viongozi wanawake wenye michango ya kuigwa juu ya usawa wa kijinsia na

uwezo wa wanawake hususani Mapambano dhidi ya mfumo dume na kuimarisha

harakati na nguvu za pamoja katika Ukombozi wa mwanamke”,aliongeza Liundi.







Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule aliwataja na

kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali ambapo Makamu

wa Rais alikabidhi tuzo kwa akina mama hao.







Miongoni waliopokea tuzo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi.

Samia Suluhu, aliyekabidhiwa tuzo yake na Mwenyekiti wa bodi.







Wengine ni pamoja na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda,

Mbunge wa Bunda Mjini, Estar Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester

Mwaikambo, na Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada

walizozionesha katika uongozi na wote walipewa tuzo. 







Tamasha hilo limeandaliwa na mashirika mbalimbali ya wanawake na haki za

binadamu,watu binafsi na wadau wengine wakiwemo Wanaharakati Vijana

(YFF),Mtandao wa wanawake na Maji,Wanasemina za Jinsia na Maendeleo

(GDSS) na Vituo vya Taarifa na Maarifa.
                 

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI HAPA CHINI




Makamu

wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (mwenye mtandio) akikata utepe

pamoja na wageni meza kuu kuashiria uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia

Tanzania la mwaka 2017










Makamu

wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (mwenye mtandio) akikata utepe

pamoja na wageni meza kuu kuashiria uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia

Tanzania la mwaka 2017.




Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kushoto) akimpongeza

Spika mstaafu mwanamke wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda (kulia) mara

baada ya kupokea tuzo yake.








Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo Mama Getrude Mongela (kulia) 
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.


                                 

Washiriki mbalimbali katika tamasha hilo.







             

Wawakilishi wa nchi mbali mbali wakitoa salam zao katika tamasha hilo




Katibu

Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Bi.

Siaba Mkinga akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha hilo.








Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akizungumza leo wakati

akizinduwa rasmi Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017. Uzinduzi huo

umefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.




Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akizungumza leo wakati

akizindua rasmi Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017. Uzinduzi huo

umefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia

kwake ni wageni waalikwa meza kuu.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akicheza na wasanii na wageni waalikwa. 
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo

mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia)
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo kwa

Zipora Shekilango (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia

Tanzania la mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo

mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marry Lusimbi (kulia) kwenye

uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.




Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo

mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu Stephen Magoiga kwa kufanikiwa

kutenga rasilimali fedha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 kuwezesha

wasichana upata taulo za kujihifadhi bure wanapokuwa kwenye hedhi wakiwa

shuleni.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri Kisarawe.











 




Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi daktari wa kwanza mwanamke Tanzania, Dk. Ester Mwaikambo (kulia).
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi mbalimbali

na shughuli za akinamama wanaharakati ngazi ya jamii za kujikwamua.
Washiriki wa Tamasha la 14 la TGNP Mtandao wakiwa katika tamasha hilo kwenye viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam
Wanawake washiriki wa Tamasha hilo wakicheza kwa furaha 
Wanawake washiriki wa tamasha la TGNP wakiwa katika tamasha hilo.


Baadhi ya washiriki wa tamasha la 14 la mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP mtandao) wakiwa katika tamasha hilo 
Wageni kutoka nchi mbali mbali 
Wanahabari wakifuatilia tamasha hilo 

Wanahabari kutoka mikoani walioshiriki tamasha hilo


TAZAMA

VIDEO MAKAMU WA RAIS MH SAMIA  ALICHOKISEMA,MWENYEKITI WA BODI TGNP

MTANDAO BI:SHULE PAMOJA NAMKURUGENZI MTENDAJI TGNP MTANDAO BI:LILIAN

LIUNDI.




Powered by Blogger.