Dereva wa Mbunge Heche avamiwa na kukatwa na shoka

Suez
Daniel Maradufu ambaye ni Dereva wa Mbunge jimbo la Tarime Vijijini
CHADEMA John Heche  akiwa amelazwa katika Wodi namba tatu kwa ajili ya
Matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.




Dereva wa
Mbunge John Heche (CHADEMA) amevamiwa usiku wa kuamkia leo Ijumaa Septemba
15,2017  na watu wasiojulikana na kukatwa na shoka kichwani Mjini Tarime ambapo
kwa  sasa hali yake inaendelea vizuri
huku akipatiwa matibau katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.


Tukio hilo limetokea jana majira ya
saa mbili usiku ambapo dereva huyo anadaiwa kukatwa na shoka kichwani
Mbunge
John Heche amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kutokana na taarifa alizopata
kupitia Katibu wake, Mrimi Zabron ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa
jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo
hospitali akipatiwa matibabu.
Mrimi
Zabron ambaye ni katibu wa Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini John
Heche  akimujulia hali  Dereva wa Mbunge  huyo katika Hospitali ya
Wilaya ya Tarime.
TAZAMA VIDEO DEREVA HUYO AKISIMULIA ALIVYOSHAMBULIWA
Powered by Blogger.