MGODI WA ACACIA BULYANHULU WATOA MSAADA WA MAGODORO KITUO CHA AFYA CHELA CHA HALMASHAURI YA MSALALA
Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu
umetoa msaada wa magodoro 14 katika kituo cha afya Chela kilichopo
katika Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa
ajili ya kuboresha huduma za afya katika wodi za wagonjwa katika kituo
hicho.
Akizungumza jana Agosti 22,2017 wakati akikabidhi magodoro hayo, Kaimu
Meneja wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bryson
Tarimo(aliyesimama pichani) alisema magodoro hayo 14 ni kwa ajili ya
wodi za wagonjwa katika hicho cha afya.
"Afya ni haki ya kila mwananchi, katika juhudi za kuchangia
uboreshaji wa huduma za afya kwenye halmashauri ya Msalala,kama wadau wa
sekta ya afya, mgodi wetu umefika katika kituo cha Chela kwa mara
nyingine tena kukabidhi magodoro haya ambayo tuliyoombwa mwaka huu
wakati wa uzinduzi wa jengo la upasuaji ambalo pia tusishiriki ujenzi
wake kupitia taasisi ya Mkapa Foundation",alieleza Tarimo
Akipokea magodoro hayo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Hamad
Nyembea aliushukuru mgodi huo kwa kutimiza ahadi yake ambayo waliitoa
kwa Mkuu wa Mkoa wakati wadau wa sekta ya afya Msalala walipokabidhi
jengo la upasuaji.
Kulia ni Kaimu Meneja wa Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Bryson
Tarimo akishikana mkono na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk.
Hamad Nyembea wakati wa kukabidhi magodoro 13 kwa ajili ya kituo cha
afya Chela
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Dk. Hamad Nyembea akizungumza
wakati wa kupokea magodoro hayo 14 yaliyotolewa na mgodi wa Bulyanhulu