Kilichoendelea Leo Mahakamani Kuhusu MKOJO wa Manji
Mkemia
kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic ameieleza
Mahakama ya Kisutu leo August 23, 2017 kuwa dawa za kulevya
(Benzodiazepines) alizobainika anatumia mfanyabiashara Yusuf Manji
zinatolewa hospitalini na zinauzwa Pharmacy.
Mkemia
huyo amesema hajui kama sampuli ya mkojo alioupima ni wa Manji ama
Askari Polisi, kwa sababu wakati Manji anachukuliwa sampuli hiyo
aliingia chooni na Askari, huku yeye akiwasubiri nje.
Aidha,
Mkemia amesema katika kipimo cha mkojo wa Manji amebaini uwepo wa dawa
aina ya Benzodiazipines ikiwa ni zao la Heroin, ambapo dawa hiyo ina
matumizi mengi ikiwemo kuondoa maumivu makali, ikitegemeana na ushauri
wa daktari.
Baada ya kuelezwa hayo, Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis amesema Serikali imefunga ushahidi wa mashahidi wake watatu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema atatoa uamuzi kama Manji ana kesi ya kujibu ama la, August 25/2017.