UMOJA WA MAKANISA WAKABIDHI VIFAATIBA HOSPITALI YA MKOA WA SIMIYU.



Baadhi ya Viti vya kubebea wagonjwa(wheel chairs) vilivyotolewa na Shirika la Madhehebu ya Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakipokea baadhi ya vifaa vilivyotolewa Life Ministry kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika hilo la dini, Bw. Dismas Shekalaghe(Kulia)


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati), Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa(kushoto) wakikabidhiwa viti vya kubebea wagonjwa na Mkurugenzi wa Life Ministry Bw. Dismas Shekalaghe (kulia). ambavyo ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa Shirika hilo la Kikristo kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, Dkt.Fredrick Mlekwa akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, mjini Bariadi
vifaa vilivyo tolewa


          Na COSATNTINE MATHIAS SIMIYU 
  Life Ministry kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya kikiristo mjini Bariadi wametoa vifaa tiba ikiwemo baiskeli za kusukuma wagonjwa na vinginevyo vitakavyosaidia kutoa huduma kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa ambazo zimegharimu zaidi ya milioni 40.

Aidha Uhaba wa Vifaa tiba katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu (Somanda) bado ni changamoto inayoikabili hospitali hiyo, hali inayofanya utoaji wa huduma za kitabibu kuwa duni.

Akiongea kabla ya kukabidhi vifaa tiba, Mkurugenzi wa Life Ministry Dismas Shekalaghe kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya kikiristu Bariadi, amesema kuwa wanatoa mchango huo ili kuipunguzia serikali mizigo ya bajeti katika mfuko wa hospitali.

Amesema kuwa madaktari na wauguzi wamekuwa wakiokoa maisha ya jamii katika kutoa matibabu na kanisa pia huwa lina mchango wake katika jamii kwa watu wanaoishi.

‘’tuna vifaa kadhaa ambavyo tumeona tuvilete hapa kama masaada tunashirikiana na umoja wa makanisa mkoa wa Simiyu…viti vya kubebea wagonjwa, vifaa vya viuongo bandia, vifaa vya huduma ya meno, vifaa vinavyotumika katika upasuaji, Bandeji na mabomba ya sindano zinafikia milioni 40 hadi 50’’ alisema Shekalaghe.

Aliongeza kuwa wanawashukuru Madaktari, Wauguzi na manesi kwa kuokoa maisha ya watu wanaofika hospitali kupata matibabu ambao wanafika hospitali kwa kukosa matibabu.

Akipokea Msaada huo kwa niaba ya serikali, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amesema kuwa katika sekta ya afya hakuna msaada mdogo kwa sababu hata hicho kidogo kinaokoa maisha ya watu.

Aidha Mtaka ameongeza kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini utatuzi wake ni wa muda mrefu kwa kuwa bado ni mpya huku ikitegemewa na wananchi wengi wanaoizunguka.

‘’tunashukuru kwa msaada uliotolewa na life ministry utaisadia hospiatali hii pia iwawashawishi madaktari kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi na ili Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawezeshwe vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na kuongeza ari ya kufanya kazi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Fredrick Mlekwa amesema kuwa msaada huyo umewafikia kwa muda mwafaka kwa kuwa wako katikati ya bajeti, utawasadia katika utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.

“Tumefarijika sana kupata msaada huu na walengwa ambao ni wananchi watapata huduma bora kupitia vifaa hivi, naomba nitoe wito kwa Mashirika mengine ya madhehebu ya dini kuendelea kutusaidia kwa kuwa Hospitali hii inawahudumia watu wenye mahitaji mbalimbali” alisema Dkt.Mlekwa.
Nao baadhi ya wananchi wameushukuru umoja wa makanisa huo kwa kuona mahitaji ya wagonjwa ambao ni waumini wao, ambavyo vitasaidia wagonjwa wa aina yeyote hata wasio na dini ili waweze kupata huduma hizo.


‘’vifaa hivi vilivyotolwa na umoja huu wa makanis awatasaidia watu wote bila kujali itikadi za dini zao, pia itakuwa ni hamsa kwa maktari na wauuguzi kufanya kazi kwa tija….alisema Sylvester Sungwa mkazi wa Sima-Bariadi.

                       
Powered by Blogger.