REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA UEFA KWA KUWACHAPA JUVENTUS BILA HURUMA
Mechi ilianza kwa kusuasua huku kila upande ukicheza kwa tahadhali kubwa
ili wasiruhusu goli lake kuguswa. Juventus wakianza mechi kwa kuonesha
ubora zaidi kwenye upande wa Ulinzi ambao uliongozwa na wakongwe kuzuia
mashambulizi ya Real, Haikumchukua muda mrefu nyota Christiano Ronaldo
aliipatia goli la kuongoza lakini baadae mshambulizi Mario Mandžukić
akaisawazishia Juventus na kufanya mchezo kuwa 1 – 1.
Mpaka
kipenga kinapulizwa kuashiria mapumziko timu zilikuwa sare kwa goli 1 –
1 huku Real Madrid wakiwa wamemiliki mpira kwa 54% na Juventus 46%.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku pande zote mbili zikijitahidi
kushambulia, Dakika ya 61 Casemiro akaiandikia Real goli la pili,
Haikuchukua muda mrefu Christiano Ronaldo akaipatia Real goli la 3
dakika ya 65 na kufanya mchezo kuwa 3 – 1 huku Golikipa wa Juventus
akionekana kukata tamaa baada ya kufugwa magoli ya haraka haraka ambayo
yalimpotezea ramani nzima ya mchezo.

Kosa kubwa walilolifanya Juventus ni kumruhusu Marcelo kuanza kutembea
na kutengeneza nafasi ambapo alipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Luka
Modrich ambao ulizaa matokeo chanya.

Dakika ya 83 Juan Cuadrado akioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu
beki wa Real Madrid Sergio Lamos na kutolewa nge hivyo Juventus kusalia
na wachezaji 10.
Goli la 4 la Real Madrid lilipachikwa na Marco Asensio na kufanya
mchezo kumalizika Real Madrid 4 huku Juventus 1 na hivyo Real Madrid
kutwaa ubingwa wa UEFA Champions League 2016/17.