Anna Mgwira kuapishwa leo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Anna Mghwira anaapishwa leo baada ya kuteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Said Meck Sadick aliyeomba kujiuzulu.
Hadi wakati huu hakuna taarifa rasmi iliyokuwa imetolewa na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wao, na wala mteule huyo hajazungumza jambo lolote.