Yanga wametua jijini Dar es Salaam wakiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara na mashabiki wao wamejitokeza kwa wingi kuwalaki. Mashabiki hao wamejitokeza kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi klabuni mwao.