Waandishi wa Mwananchi Communication
limited inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti mkoani
Mara wamekuwa mfano wa kuigwa kutokana na weledi wa kazi zao.
Sifa hizo zilitolewa mwishoni mwa
wiki katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari uliofanyika
mkoani mara mjini Musoma kwa kutajwa kuwa waandishi mahiri wa habari za
uchunguzi na makala.
Waliotajwa kuwania mfano wa kuigwa
ni Dinna Maningo, Antony Mayunga wa Mwananchi na Beldina Nyakeke wa the
Citizen.
Akitoa salama za siku hiyo mkuu wa
wilaya ya Musoma Dr. Vicent Aneyi alisema kuwa amekuwa akisoma kazi zao lakini
hakuwahi kubahatika kuwaona.
"Leo ni siku njema kwa
kuwafanya nimeona na Dinna na Mayunga ambao ni watu wa kawaida
lakini wenye mawazo mapana,nimekuwa nikisoma habari zao lakini sikuwahi kuwaona
,wana mawazo chanya ambayo yanatakiwa kuigwa na waandishi wengine,"alisema
Mkuu huyo wa Wilaya.
Awali mwenyekiti wa chama cha
waandishi wa habari mkoani Mara (MRPC)
Mugini Jacob alisema kampuni ya Mwananchi imekuwa mfano wa kuigwa kwa waandishi
wake kuandika habari za uchunguzi na kutwaa tuzo zinazotolewa na taasisi
mbalimbali zinazojihusisha na habari ukiwemo mfuko wa kufadhili waandishi Tanzania
(TMF).
"Tuna fursa za kugeukia habari
za uwekezaji katika mkoa wetu ili tuweze kufanya wawekezaji kuona fursa
zilizoko mkoa hapa waje kuwekeza, naamini kupitia kalamu zetu tunaweza kufanya
sura ya mkoa wetu ukawa na matukio makubwa ya kiviwanda,"alisema Jacob
ambaye ni mwandishi wa gazeti la serikali ya kiingereza Daily news.
Wakizungumza katika maadhimisho hayo
waandishi wa Mwananchi Dinna Maningo na Antony Mayunga walisema ipo haja ya
kufanya mabadiliko katika uandishi wa habari kuwa wa kitakwimu.
"Sasa ni wakati wa kuandika
habari za kitakwimu (data journalism) na hii itatusaidia hata kuandaa maswali
wakati wa kufanya mahojiano na !asali hayo yatakuelekeza ni nani anapaswa
kuyajibu ili kupata takwimu hizo,'alisema Mayunga.
Aidha Maningo aliwataka waandishi
mkoani Mara kufanya uandishi wa uchunguzi na kuachana na mialiko.
"Ukifanya habari za uchunguzi
huwezi mlalamikiwa mkuu wa mkoa au wilaya kuwa hukualikwa kwenye kikao chake
kwani utakuwa na kazi nyingi za kufanya ambazo zitakuwa heshima na wakati
mwingine viongozi wa serikali watakuta taarifa ambazo wanazihitaji, nimekuwa
mnufaika wa mfuko wa TMF tangu 2012 hadi mwaka 2016 ambao hulipwa kuanzia
sh,milioni hadi sh, 4 milioni," alisema Maningo.
Siku ya uhuru wa vyombo vya habari
Tanzania huungana na nchi nyingine dunia kuadhimisha kila mei 3, ambapo mkoa wa
Mara kauli mbiu yake ilikuwa 'Sasa ni wakati wa habari za uwekezaji wa viwanda.
|