WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO TANZANIA WAKUTANA JIJINI MWANZA KUPANGA MIKAKATI.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na
waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika
Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza juzi ili kujadili masuala
mbalimbali ya chama hicho.
Katibu wa Chama hicho, Elias Msuya akizungumza katika kikao hicho. Kulia ni Mtunza Fedha wa chama hicho, Ellen Manyangu.
Wanachama wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Mwanza
Waandishi wa
Habari wanaounda Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo wamekutana
Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo
mbalimbali ya chama hicho.
Akizungumza
katika kikao hicho, Mwenyekiti wa chama hicho, Gerald Kitabu pamoja na
mambo mengine alihimiza wanachama ambao bado hawajatoa michango yao ya
mwaka waitoe ili kutunisha mfuko wa chama hicho.
"Ni muhimu wanachama ambao bado hawajaotoa michango yao kuhakikisha wanaitoa kwa wakati" alisema Kitabu.
Katibu wa Chama
hicho, Elias Msuya alisema chama hicho kipo katika mchakato wa
kutengeneza vitambulisho kwa ajili ya wanachama na wakati wowote
vitakapo kuwa tayari vitatolewa kwa wahusika.