TBS YAWASHAURI WAZALISHAJI WADOGO WADOGO WA BIDHAA KUTUMIA FURSA YA BURE YA UKAGUZI.
Wazalishaji wadogo
wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi
wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.
Hayo yamesemwa na
Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka
pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye
maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .
Alisema kuwa licha
ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati
wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha
kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
"Bado wazalishaji
wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia
kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza
bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa"
alisema Kaseka.
Aidha alisema kuwa
bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha katika soko
bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara katika
masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.
Nae Mfanyabiashara
Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano wa bidhaa
kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi tofauti na
wanazozizalisha.
Alisema kuwa iwapo
TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka nje
utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa kuweka
nembo bidhaa zao.
Na Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.