Na
Nuru Juma, Husna Saidi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aahidi nyongeza ya
kawaida kwa mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi wanaostahili.
Rais
Magufuli ametoa ahadi hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku
ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chuo Cha
Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Dkt.
Magufuli alisema Serikali ilisitisha upandishaji wa vyeo na mishahara kutokana
na kuwepo na watumishi hewa na walioghushi vyeti lakini baada ya kuondolewa Serikali
itahakikisha inashughulikia maslahi ya wafanyakazi.
“Watumishi
9932 walikuwa na vyeti feki,watumishi hewa walikuwa 19706 hivyo kama Serikali
ingeongeza mishahara inamaana watumishi hawa pia wangefaidika na pesa ambazo
hawakustahili kuzipata”, alisema Dkt. Magufuli.
Aidha
aliwataka waajiri kuheshimu na kutoa mikataba ya kazi na kutowanyanyasa wafanya
kazi wao na wafanyakazi kuomba kazi kulingana na elimu zao na waache tabia ya
kughushi vyeti.
Aliongeza
kuwa Serikali itashughulikia mfumuko wa bei za bidhaa na kuhakikisha viwanda
vingi vitajengwa sehemu mbalimbali nchini ili kuongeza ajira kwa vijana wa
kitanzania.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TUCTA Dkt. Yahya Msigwa ameipongeza Serikali kwa
kutekeleza ahadi zake na kuopngeza kuwa hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali
inayodhamira ya dhati ya kuwajali wananchi wake wakiwemo wafanyakazi.
Ameongeza
kuwa wanayo imani kubwa kwa Serikali kuwa itatekeleza ahadi yake ya kufanyia
maboresho ya maslahi ya umma kama ambavyo umeonyesha nia njema ya kutekeleza
ahadi zake.
Alizitaja
baadhi ya ahadi zilizotekelezwa kuwa ni pamoja, kupiga vita rushwa na ufisadi,
kuondoa watumishi hewa, Serikali kuhamia Dodoma, ujenzi wa miundombinu ya reli,
vita dhidi ya dawa za kulevya pamoja na ununuzi wa ndege.
“Ni
imani yetu kuwa ahadi hii ya kuboresha maslahi kwa Watumishi wa Umma
itatekelezwa kwa wakati kwani tayari umekwisha ondoa mambo yaliyokuwa
yanakwamisha zoezi hilo,” alisema Dkt. Msigwa.
Wakati
huohuo Katibu Mkuu huyo ameiomba Serikali kuharakisha kubuni namna ambavyo
wafanyakazi watanufaika na Mifuko ya Jamii na wanaodai mapato yao kusikilizwa
kesi zao kwa wakati.
Maadhimisho
hayo yameuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai,Naibu Spika Tulia Ackson, Mawaziri Jenister Mhagama na Angella Kairuki,
Profesa Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na
baadhi ya Wabunge. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Uchumi wa Viwanda Vizingatie Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi”.
|