SABABU ZA KUPOROMOKA KWA KILIMO CHA PAMBA GEITA ZATAJWA.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya
Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza na waandishi wa habari,
walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni
(OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye
tija kwa maofisa ugani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi
akizungumza na ujumbe huo.
Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa
Wilaya Mbogwe, Stephen Shilemba, akizungumza katika mafunzo ya siku moja
ya maofisa ugani yaliyoendeshwa na COSTECH na OFAB.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Mbogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania, Philbert Nyinondi (kushoto), akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Katibu Tawala wa
Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahali (katikati), akifungua mafunzo hayo
kwa niaba ya mkurugenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Wilayani humo, Deus Lyankando na Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Geita, David Makabila.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani humo, Deus Lyankando na Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza katika mafunzo hayo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Amina Kanyogoto.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo, Vicent Busiga (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mtaalamu wa mazao ya mizizi kutka Kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru Mwanza, Dk.Simon Jeremiah akitoa
mada kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo.
Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiliguru, Stellah Chirimi (kulia), akitoa mada.
Mkulima wa pamba, Magua Mayala
(kulia),mkazi wa Kitongoji cha Kakumbi Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe
mkoani Geita akizungumza na waandishi wa habari jana, walioongozana na
wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB)
waliopo mkoani humo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa
maofisa ugani.
Mkulima wa Kijiji cha Kakumbi, Said
Tangawizi (kushoto), akiwaonesha maofisa kilimo hao eneo ambalo linafaa
kwa shamba la mihogo la mfano.
Mkulima wa Kijiji
cha Kakumbi, Said Tangawizi (kushoto), akihojiwa na waandishi wa habari
kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo cha mhogo, mpunga,mahindi na viazi
lishe.
Watafiti
na wanahabari wakitoka kuangalia shamba la mpunga la mkulima, Said
Tangawizi. Wa kwanza kushoto ni Mshauri wa OFAB, Dk.Nicholaus Nyange,
Stellah Chirimi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiliguru, Ofisa
Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF nchini Kenya, Suleiman Okoth,
Mwandishi wa Habari, Fatma Abdu na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Kilimo Tanzania (TAJAF), Gelard Kitabu.
Na Dotto Mwaibale, Mbogwe
KUCHELEWA
kufikishwa kwa pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima wa pamba
imeelezwa kuwa kunachangia kuporomosha kilimo hicho wilayani Mbogwe
mkoani Geita.
Hayo yalielezwa
wilayani humo jana na Magua Mayala, mkulima wa pamba wa Kitongoji cha
Kakumbi Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe mkoani Geita wakati akizungumza
na waandishi wa habari walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la
Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani humo kwa ziara ya
kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.
Mayala alisema
changamoto kubwa waliyonayo wakulima katika wilaya hiyo ni
kucheleweshewa pembejeo hali inayowafanya waende kutafuta mbegu ambazo
hazina ubora ambazo zinawasababishia wakulima kupata mavuno kidogo
ukilinganisha na maeneo ambayo wanapata mbegu bora.
"Tunaiomba
serikali itusaidie kutufikishia pembejeo za kilimo kwa wakati ili
kuliinua zao la pamba ambalo ni la biashara katika wilaya yetu" alisema
Mayala.
Alisema
alipanda ekari moja ya pamba kwa kutumia mbegu duni ambapo alipata kilo
100 alizouza sh. 200,000 na kueleza kuwa changamoto kubwa ni pamoja na
dawa za kuulia wadudu waharibifu wa pamba na hata wakipata dawa hizo
haziui wadudu.
Mtaalamu wa
magonjwa ya mazao hasa ya pamba kutoka kituo cha utafiti wa kilimo
Ukiliguru, Stellah Chirimi aliwataka wakulima kuzingatia kilimo chenye
tija kwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuachana na kilimo cha
mazoea.
Katibu Tawala
wa Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahali aliwataka maofisa ugani wa
wilaya hiyo kwenda kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo na kuwaelekeza
badala ya kukaa mjini jambo ambalo litaongeza uzalishaji wa chakula.
Mwenyekiti wa
Halmshauri ya Wilaya hiyo, Vicent Busiga aliwapongeza maofisa ugani kwa
jitihada zao wanazofanya za kuwafikia wakulima licha ya kukabiliwa na
changamoto ya umbali wa kutoka eneo moja kwenda lingine kutokana na
kukoseka kwa usafiri.
Mshauri wa
Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange
alisema matumizi ya teknolojia ya bioteknolojia katika kilimo ni muhimu
kwani katika nchi za wenzetu wanaoitumia kama, Mali, Burki Faso na Misri
zimepiga hatua kubwa.
"Nchi kama
Burkina Faso imepiga hatua kubwa ya kilimo cha zao la pamba baada ya
kuamua kutumia mbegu zenye vinasaba (GMO), ambazo Tanzania hazikubaliki
na hivi sasa inazalisha wastani wa tani 2.9 kwa hekta ambapo nchi zote
za Afrika zinakwenda kujifunza kwao kuhusu kilimo cha pamba" alisema
Nyange.