RAIS DKT MAGUFULI ATEUA NAIBU KAMISHINA MKUU TRA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Uteuzi wa Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza tarehe 22 Mei, 2017.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.
Bw.
Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna
Mkuu wa TRA.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam