PICHA YA MWISHO YA SHABIKI WA SIMBA, ALISHANGILIA NA MUSSA MGOSI NA MASHABIKI WENGINE
Marehemu Shose Fidelis alikuwa shabiki
wa Simba hasa, ndiyo maana akaamua kufunga safari hadi Dodoma kuiunga
mkono timu yake ikipambana na Mbao FC katika mechi ya fainali ya Kombe
la Shirikisho.
Simba imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1
na kubeba ubingwa, lakini furaha ya Shose imeishia Dumila Morogoro
baada ya kupata ajali ya gari ambalo pia lilikuwa limembeba Nahodha wa
Simba, Jonas Mkude.
Katika akaunti yake ya Isntagram,
inaonyesha Shose alitupia picha mbili tu jana. Ikionekana moja kabla ya
mechi ya fainali na nyingine baada ya mechi hiyo.
Picha baada ya mechi anaonekana akiwa na Meneja wa Simba, Mussa Mgosi na mashabiki wengine wa Simba.