MKUDE ANUSURIKA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI, MMOJA APOTEZA MAISHA
Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amepata ajali baya ya gari.
Mkude
alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba
kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la
Shirikisho.
Mkude alikuwa katika gari na baadhi ya mashabiki wa Simba na gari lilipasuka tairi na kuanguka. Mtu mmoja amefariki dunia.