Picha: RC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU WA SEKTA YA AFYA,AZUNGUMZIA UGONJWA WA EBOLA
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewataka wadau wa afya mkoani
Shinyanga kufanya kazi kwa uwazi ili kuepuka migongano inayoweza
kujitokeza wanapotekeleza majukumu yao katika jamii.
Telack ameyasema hayo leo Jumanne May
30,2017 wakati akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa sekta ya afya
mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa
wa Shinyanga.
Telack alisema ili kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ni vyema wadau
wakatekeleza majukumu yao kwa uwazi lakini pia taasisi na mashirika
mbalimbali kujitambulisha serikalini kabla ya kuanza kutekeleza majukumu
yao katika jamii.
“Mkoa wa Shinyanga una wadau wengi wa
afya,naomba mfanye kazi kwa uwazi na kuzingatia maadili,lakini pia ni
vyema kabla hujaanza kutekeleza mradi jitambulishe kwa viongozi wa
serikali”,alieleza Telack.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa
alimtaka mganga mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua tahadhali kuhusu
tishio la ugonjwa wa Ebola kwani wilaya hiyo ina mwingiliano wa watu
wengi na wataalam wa afya wahakikishe wanatoa taarifa mara moja endapo
mtu yeyote atabainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.
“Ugonjwa huu umeripotiwa kuwepo
katika nchi jirani ya Congo ,hapa kwetu bado hatujapata taarifa za
kuwepo mgonjwa wa ebola,niwaombe pia wataalam wa afya maeneo yote ya
mkoa wa Shinyanga kuchukua tahadhali juu ya ugonjwa huu”,aliongeza.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume aliwaondoa hofu wakazi wa mkoa wa Shinyanga
kuwa ugonjwa huo haujaingia mkoani humo na kuongeza kuwa tayari
wameanza kuchukua tahadhali juu ya tishio la ugonjwa huo.
Dkt. Mfaume alitumia fursa hiyo kuwaomba
wadau wa afya kujitokeza kusaidia katika masuala ya dharura
yanapojitokeza badala ya kujikita katika sera za taasisi ama mashirika
wanayofanyia kazi.
Naye Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga
Albert Msovela alisema lengo la kikao hicho cha siku mbili cha wadau wa
afya mkoa wa Shinyanga ni kuwaleta pamoja wadau wanaoshughulika na
masuala ya afya ili kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya afya na
namna ya kuzitatua lakini pia kufahamiana.
Miongoni mwa wadau waliohudhuria kikao
hicho ni pamoja na viongozi ngazi ya mkoa,halmashauri za wilaya,Shirika
la Intrahealth International,CUAMM,Save the Children,JHPIEGO ,TAWLAE,Red
cross,AGPAHI,World vision,ICS,PSI,AGAPE,Pathfinder International,Good
Neighbors,USAID,TAMA,IMA,Amref International,HPSS na wengine wengi.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama
Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kikao cha wadau
wa afya mkoa wa Shinyanga siku ya kwanza May 30,2017…Tazama hapa chini
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt.
Rashid Mfaume akitambulisha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga
Albert Msovela akimkaribisha mgeni rasmi,mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainab Telack akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa afya mkoa wa
Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akifungua kikao cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Wadau wa afya wakiwa ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua kikao cha wadau wa afya
Kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa
Shinyanga Albert Msovela akiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa
Shinyanga,Glory Mbia wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Kikao kinaendelea
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizungumza ukumbini
Wadau wa afya wakiwa ukumbini,kulia ni Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dkt. Joseph Ngowi
Kushoto ni Mratibu wa Ubia na Sekta
Binafsi mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Isaac Mzee akiwa na mratibu wa
huduma za maabara mkoa wa Shinyanga Muhdin Hamza
Afisa Lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madereke akitoa mada
Mratibu wa afya ya Mama na Mtoto mkoa wa Shinyanga Joyce Kondoro akitoa mada
Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lydia Kwerigwabe akitoa mada ukumbini
Kikao kinaendelea
Mwakilishi wa Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Ansila Benedict akitoa mada katika kikao hicho
Mwakilishi wa shirika la CUAMM, Arianna Bortolani akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo
Afisa Tiba na Matunzo kutoka shirika la AGPAHI Fidelis Temba akielezea kazi zinazofanywa na shirika hilo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
Afisa Tiba na Matunzo kutoka shirika la AGPAHI Fidelis Temba akielezea kazi zinazofanywa na shirika hilo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
Wadau wakifuatilia mada ukumbini
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Mjumbe akitoa mada kuhusu mfumo wa jazia dawa
Mwakilishi kutoka shirika la Intrahealth International akitoa mada
KIKAO KINAENDELEA,TUTAWALETEA PICHA ZAIDI HIVI PUNDE...
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog