Picha: RAIS MAGUFULI AKABIDHI HATI KWA WAFANYAKAZI BORA ACACIA,WASHIRIKI MAANDAMANO MEI MOSI 2017
Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi
Tanzania (TUCTA) limewatunuku hati ya Mfanyakazi Bora wafanyakazi watatu
kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na
Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia.
Waliotunukiwa hati ya mfanyakazi bora
2017 na zawadi ya shilingi milioni 1.5 kila mmoja ni Elisante Okuli
Mungure kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,Masule Sangalali na Shaban
Nassoro Katala kutoka mgodi wa Buzwagi.
Wafanyakazi hao wamekabidhiwa hati hizo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
wakati wa Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi 2017’ambayo kitaifa
imefanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi mkoani
Shinyanga.
Bwana Elisante Okuli Mungure anafanya
kazi Huduma za kitaalamu kwenye uchimbaji wa madini (Technical Service)
katika mgodi wa Bulyanhulu na Masule Sangalali ni Fundi mitambo katika
mgodi wa Buzwagi wakati Shaban Nassoro Katala anafanya kazi ya uchimbaji
katika mgodi wa Buzwagi.
Wafanyakazi hao wametunukiwa hati ya
mfanyakazi bora na TUCTA kwa ajili ya kazi bora,utii na kufuata maongozi
sahihi katika kutimiza wajibu wa ujenzi wa taifa la Tanzania mwaka
2017.
Wafanyakazi wa Acacia wameshiriki siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi 2017’
kwa kufanya maonesho ya kazi wanazofanya mgodini lakini pia wameshiriki
maandamano yaliyofanywa na wafanyakazi nchini mbele ya rais Magufuli.
Nimekuwekea hapa chini picha za matukio yaliyojiri wakati wa siku ya wafanyakazi duniani leo Jumatatu Mei Mosi 2017.
Bwana Elisante Okuli Mungure kutoka
mgodi wa Bulyanhulu akipokea hati ya Mfanyakazi bora mwaka 2017 katika
viwanja vya ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa sherehe za Mei
Mosi.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka mgodi wa
Bulyanhulu wakifurahia baada ya mfanyakazi mwenzao Elisante Okuli
Mungure kutajwa kuwa ni Mfanyakazi Bora mwaka 2017
Elisante Okuli Mungure akionesha hati aliyopewa
Elisante Okuli Mungure akiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni bwana Masule Sangalali ambaye
ni fundi mitambo katika mgodi wa Buzwagi na Shaban Nassoro Katala
anayefanya kazi ya uchimbaji katika mgodi wa Buzwagi wakionesha hati zao
za Mfanyakazi Bora mwaka 2017
Masule Sangalali na Shaban Nassoro Katala wakionesha hati zao za ushindi
Kushoto ni Elisante Okuli Mungure kutoka
mgodi wa Bulyanhulu ,katikati ni Masule Sangalali na Shaban Nassoro
Katala wakionesha hati zao za ushindi
Wafanyakazi wa kampuni ya Uchimbaji
madini ya Acacia inayomiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi,North Mara na
Bulyanhulu wakiwa wamebeba bango wakati wa sherehe za Mei Mosi 2017
katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani KilimanjaroRais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
maandamano ya wafanyakazi katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro wakati wa sherehe za Mei Mosi mwaka 2017.
Wafanyakazi wa kampuni ya Uchimbaji madini ya Acacia wakiandamana kwenye sherehe za Mei Mosi 2017
Bango likiwa na kauli mbiu ya Mei Mosi 2017 ' Uchumi wa viwanda uzingatie haki,maslahi na heshima ya wafanyakazi'
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa wamebeba bango
Maandamano yanaendelea
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa katika maandamano
Maandamano yanaendelea
Baadhi ya wabunge wakiwa jukwaani
Baadhi ya wafanyakazi wa Acacia wakiwa jukwaani
Muonekano wa banda la kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Wananchi wakiwa katika banda la Acacia
kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa kampuni
hiyo inayomiliki migodi ya Buzwagi,North Mara na Bulyanhulu
Wananchi wakiwa katika banda la Acacia
Afisa kutoka Acacia akitoa maelezo kuhusu vifaa vya uokoaji mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la Acacia
Wanafunzi wakiwa katika banda la Acacia kujifunza masuala ya migodi
Maonesho ya Mei Mosi 2017 katika banda la Acacia yakiendelea
Aprili 30,2017-Wafanyakazi wa kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Ushirika Moshi
Picha ya pamoja
Wafanyakazi wa Acacia katika picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog