KAULI ZA RAIS MAGUFULI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI - MEI MOSI 2017


YALIYOJIRI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI) 2017 KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA USHIRIKA MOSHI,MKOANI KILIMANJARO
#Tunakushukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo suala la elimu bure nchini - Said Meck Sadik.
#Kati ya walimu wa Sayansi 100 waliopangikiwa mkoa wa Kilimanjaro, 94 wamesharipoti - Said Meck Sadik.
#Serikali ya Mkoa imekuwa ikisisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi mahala pa kazi - Said Meck Sadik.
# Changamoto ya ukosefu wa ajira ni la tatizo la Dunia na Tanzania ni moja ya nchi inayokabiliwa na tatizo hilo - Mkurugenzi ILO.
#Kwa jitihada zinazofanywa na serikali, tunaona uchumi wa kati uko karibu - Mkurugenzi ILO.
# Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kwa ukaribu na TUCTA na ATE - Jenista Mhagama.
#Tucta inaishauri Serikali kufuata sheria za kazi katika kuwachukulia hatua wafanyakazi - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Tunaishauri Serikali kuharakisha uboreshaji wa mifuko ya jamii ili wafanyakazi waanze kunufaika - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Wapo waajiri ambao wanakiuka sheria za kazi, mfano kunyanyasa watumishi na kutoa kazi kwa ndugu zao - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Tunaiomba Serikali kupandisha kima cha chini cha mshahara unaokatwa kodi kufikia 750,000/-. - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Tucta inawakumbusha wafanyakazi kutimiza wajibu wao sehemu za kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Si wajibu wa Tucta kutetea uovu kama vile ulevi, ubadhilifu na utoro sehemu za kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Tunaipongeza Serikali kwa kusisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.
#Tunakushukuru Mhe. Rais kwa kubali kuwa mgeni wetu rasmi wa siku hii ya leo - Tumaini Nyamhokwa - Rais TUCTA.
#Siku ya Wafanyakazi Duniani ni siku muhimu kwa wafanyakazi kutafakari masuala yanayowahusu - Rais Magufuli.
#Wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika taifa lolote duniani - Rais Magufuli.
#Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wafanyakazi - Rais Magufuli.
#Nawahakikishia wafanyakazi kuwa tunaanza ukurasa mpya kwani serikali tumeamua kwenda mbele - Rais Magufuli.
#Nawaarifu kuwa serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya Ajira na wadau wameshatoa maoni - Rais Magufuli.
#Serikali inalishughulikia suala la ucheleweshaji wa mafao ili wafanyakazi wanapostaafu waache kuhangaika - Rais Magufuli.
#Vyama vya Wafanyakazi ni mahala pa kazi na sio hiari na visigeuzwe sehemu ya migogoro - Rais Magufuli.
#Waajiri wote wanatakiwa watoe mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kinyume na hapo ni kuvunja sheria - Rais Magufuli.
#Serikali itaendelea kusaini na kuridhia mikataba ya kimataifa wafanyakazi yenye maslahi kwa wafanyakazi - Rais Magufuli.
#TUCTA endeleeni kuwaelimisha wafanyakazi ili fedha za bodi ya mikopo ya elimu ya juu ikusanywe kikamilifu - Rais Magufuli
#Tumebaini watumishi hewa 19706 waliokuwa wanaisababishia serikali hasara ya Tsh Bil. 230 kwa mwaka katika misharaha peke yake - Rais Magufuli.
#Serikali itashughulikia suala la mfumuko wa bei ili kuondokana na ugumu wa maisha - Rais Magufuli.
#Wapo walio na umri wa kustaafu lakini hawataki kuondoka hawa nao tutaanza kuwafuatilia, hawana tofauti na watumishi hewa - Rais Magufuli
#Nilitaka nisafishe kwanza kabla ya kupandisha mishahara kwa wafanyakazi ili tusiwafaidishe wasiostahili - Rais Magufuli.
#Nawaahidi tutatoa ajira 52000 katika sekta mbalimbali baada ya kutoa watumishi hewa na walio na vyeti feki - Rais Magufuli.
#Yeyote atakayehamishwa hakuna kuhama mpaka ulipwe hela ya kuhamishwa - Rais Magufuli.
#Serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wafanyakazi na haitadharau wala kupuuza maombi yenu - Rais Magufuli
#Niwaahidi wafanyakazi kuanzia bajeti ijayo tutaongeza mishahara kutoka kiwango kilichokaa kwa muda mrefu - Rais Magufuli.
#Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi pamoja na kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja yake - Rais Magufuli.
#Serikali hii itakuwa mtetezi namba moja kwa wafanyakazi - Rais Magufuli.
#Nikitoka hapa nitakaa na Baraza la Mawaziri ili kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi - Rais Magufuli.
#Kwa sheria zote zitakazoletwa kama miswada tutafanyia kazi kwa wakati ili mambo yenu yaende vizuri - Spika Job Ndugai
#Nasisitiza msiwahamishe wafanyakazi kabla hamjawalipa stahili zao - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO 
[09:14, 5/1/2017] Chibura Uhuru: Muhtasari wa hotuba ya Rais hii leo huko mkoani Kilimanjaro kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani!.
1.Ujenzi wa reli,ndege,elimu bure unalenga kulijenga taifa letu na kuwasaidia wafanyakazi.
2.Serikali inapochukua hatua kama za kubana matumizi na mianya ya ukwepaji wa kodi nia ni kuleta maendeleo!.
3.Serikali inapoongeza bajeti ya maendeleo,afya,maji n.k nia ni kuleta maendeleo kwa watanzania!.
4.Kuanzishwa kwa fao la kutokuwa na ajira,muswada upo njiani kupelekwa bungeni!.
5.Kuhusu kuwepo kwa mifuko ya jamii isiyozidi miwili,serikali imeridhia wazo hilo la kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ili ibaki miwili,mchakato upo katika hatua ya baraza la mawaziri!.
6.Serikali sasa itakuwa inawasikisha michango yake kwa wakati kwenye mifuko ya jamii,wakati serikali ya awamu ya tano
inaingia madarakani ilikuwa inadaiwa shilingi Trilion1.4,ambapo mpaka sasa serikali imepunguza deni kwa kulipa kiasi cha Trilion 1.3.
7.Kuhusu usalama kazini(Afya na ugonjwa wa ukimwi),uhuru wa wafanyakazi kujiunga na vyama vyao,haya yote yapo kwa mujibu wa sheria,kuhusu vyama vya wafanyakazi,vyama hivi pamoja na kuwepo kisheria,visigeuzwe kuwa chanzo cha migogoro na migono!.
8.Kuhusu mikataba ya ajira kwa wafanyakazi,waajiri wote wanapaswa kutoa mikataba ya ajira kwa watumishi wao!.
9.Kuhusu mikataba ya kazi ya kimataifa,serikali imeahidi kuendelea kusaini na kutekeleza mikataba yote ya kimataifa,serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa vitambulishi na ule wa mabaharia!.
10.Kuhusu ugumu wa maisha na mfumuko wa bei,Rais amewahakikishia wafanyakazi kuwa serikalini inakifanyia kazi,kwa sasa mfumuko ni asilimia 6.
11.Kuhusu makato ya mishahara kwenye mikopo ya elimu ya juu,serikali imesema urudishaji wa mikopo umekuwa wa kusuasua wakati idadi ya wanufaika ikipanda,serikali haiwezi kuendelea kukopesha wakati wadaiwa wakiwa wazito kurejesha mikopo hiyo!.Kila aliyekopa lazima alipe!.
12.Kuhusu sekta ya viwanda,serikali imedhamiria kufufua viwanda vyote vilivyokufa,serikali ya awamu ya tano imedhamiria kulivalia njuga suala la viwanda!.
13.Mifuko ya jamii sasa imeelekeza kwenye ujenzi wa viwanda(sukari morogoro,viatu Moshi n.k).
14.Kuhusu maslahi ya wafanyakazi,serikali lazima ichukue hatua kadhaa kabla ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi,mpaka sasa kuna watumishi hewa 19,796,Serikali ilikuwa inapoteza kiasi cha shilingi bilioni 230 kwa mwaka kwa kulipa mishahara kwa watumishi hewa,
15.Serikali inaendelea kuhakiki uongo wa watumishi wa umma walioodanganya kuhusu umri,kuna watu wengi wamedanganya umri,wana umri zaidi ya miaka 60.
16.Wapo wenye vyeti feki,wamebainika watumishi degree feki,serikali imesisisitiza kila mtu aombe kazi kulingana na elimu yake halali,Rais kasema kuna watu wakubwa wana vyeti vya kufoji!.Katika wafanyakazi laki nne waliohakikiwa elfu 9 wanavyeti vya kufoji,1500 vyeti vyao vinatumika zaidi ya watumishi wawili!.
17.Wenye vyeti feki wajiondoe wenyewe,kuna watoto wa viongozi wamefoji vyeti.
18.Serikali ilisitisha zoezi la ajira na upandishaji wa mishahara ili kupisha zoezi la kuhakiki idadi na sifa za watumishi wa umma,wale wote wenye vyeti feki,ikifika trh 15.5.2017 wawe wamejiondoa kwenye utumishi!
19.Mwaka huu wa fedha serikali itaajiri wafanyakazi wapya 52,000,baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki!.
20.Kumekuwa na tabia ya walimu kupata uhamisho ili walipwe mafao ya uhamisho,kuanzia sasa ni marufuku kuhama mpaka uwe umelipwa pesa ya uhamisho!.
21.Serikali imeendelea kulipa madeni kwa watu wote wanaotoa huduma kwa serikali,kiasi cha Trilion 3,zimeshalipwa mpaka sasa!.
22.Serikali sasa itanunua ndege sita kwa mpigo kwa gharama kubwa,ndege itakayoingia mwakani itabeba wateja 262,inauwezo wa kuruka kutoka Marekani mpaka Kilimanjaro!.
23.Mara baada ya kufungua ubalozi wa Israel,jumla ya watalii 800 walikuja nchini huku wengine 300 wakitarajiwa kuja nchini kutoka Israel.
24.Mwaka ujao wa fedha serikali itaongeza mishahara,promotion zitarejea kwa watumishi wa umma,

Powered by Blogger.