MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO.
Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika
mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa
na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa
hilo.
Mtaalamu wa
magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru
jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akizungumza katika mafunzo hayo.
Ofisa Ugani kutoka Kata ya Luharanyogu, Aminiel John, akichangia mada.
Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Buchosa, Nyabange Theopista akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa.
Maofisa Ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya
Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano
huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.
Mkutano ukiendelea.
Usikivu katika semina hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa, Kelvin Rweitaka akifungua semina hiyo kwani niaba ya mkurugenzi.
Taswira ya chumba cha mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.
Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa
magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru,
Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja
kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani
Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa
manufaa ya kilimo (OFAB).
"Ni vema kila ofisa ugani akawa na
shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo
bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya
mfano.
Katika hatua nyingine Chirimi alisema
uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa
kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha
kisasa.
Alisema kuna kila sababu ya kutolewa
elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza
tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa
viwanda hapa nchini.
Alisema hadi leo hii kuna mbegu bora
moja tu inayotumika kwa wakulima ambayo aliitaja kuwa ni UKM 08 ambayo
ikitunzwa na kuhifadhiwa vizuri itakuwa na uwezo wa kutoa kilo 700 hadi
800 kwa ekari moja.
Alisema kuwa pamoja na kuwa na mbegu hiyo changamoto kubwa iliyopo bado haijawafikia wakulima wote wa zao hilo la biashara.
Chirimi aliwata wakulima wa zao hilo
kuacha kufanya kilimo cha mazoea badala yake wafanya kilimo chenye tija
kwa kufuata maelekezo ya watafiti na maofisa ugani.
Akitoa mada katika mafunzo hayo Mshauri
wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange alisema
matumizi ya bioteknojia katika kilimo ni muhimu katika uzalishaji wa
mazao yenye tija.
Alisema nchi zinatotumia teknojia hiyo katika kilimo zimefanikiwa katika kilimo na kuwakomboa wakulima.
Alisema changamoto kubwa iliyopo kwa
wakulima hapa nchini ni mazao yao kukumbwa na magonjwa kama mnyauko wa
migomba, funza wa vitumba katika pamba, batobato na michirizi ya
kikahawia katika mihogo na ukame ambao unasababisha mahindi kunyauka na
kuwa tatizo hilo la ukame si kwa Tanzania pekee bali lipo na nchi za
jirani za Afrika Mashariki.
Ofisa Ugani wa Kata ya Nyakalilo, Mariam
Alex alisema katika kata yake changamoto kubwa ni wadudu waharibifu wa
mazao ambapo licha ya kutumia dawa mbalimbali za kuwaua lakini bado
hawajafanikiwa.
Alisema anaamini kupitia mafunzo
waliopata kuhusu kilimo yanaweza kuonesha njia ya kukabiliana na
changamoto hiyo kubwa waliyonayo.