KUMBUKUMBU YA MIAKA 21 YA MV.BUKOBA MWAKA HUU 2017.
Mei 21, 1996 taifa la Tanzania liligubikwa na msiba mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na msiba huo ambao uliyagharimu maisha ya mamia ya wapendwa wetu, baada ya meli ya Mv.Bukoba kuzama, hatua chache kabla ya kutua nanga mkoani Mwanza ikitokea mkoani Kagera.
Meli
ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani
850 na abiria 430 ilizama katika maji ya Ziwa Victoria Jijini Mwanza
yapata umbali wa kilomita 30 kutoka ufukweni mwa maji.
Ajali hiyo ilisababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika meli hiyo ambayo tangu kuundwa hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17.
Jambo la butwaa hapa ni idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na uwezo uwezo wa meli hiyo wa kubeba abiria wapatao 430.
Ajali hiyo ilisababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika meli hiyo ambayo tangu kuundwa hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17.
Jambo la butwaa hapa ni idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na uwezo uwezo wa meli hiyo wa kubeba abiria wapatao 430.
Pengine
tumezoea kwamba Mei 21 kila mwaka watanzania tunakumbuka kuzama kwa
meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya mji wa Mwanza, kwani kwa
waliokuwepo mwaka huo walipigwa na butwaa baada ya uwanja mkongwe wa
Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa shughuli za kimichezo, pale
ulipogeuka na ghafla na kutapakaa maiti za wapendwa wetu, ama hakika
inauma sana.
Wakati
mwaka huu 2017 tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni
mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja kama ilivyo imani ya watalaamu wa
masuala ya usafiri kwamba duniani kwamba usafiri wa majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je kwa Tanzania imani hiyo ina
mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.
Lakini
wakati tunatafakari suala hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe
bila kusubiri kusukumwa na mtu hususani wale wenye mamlaka ya kuleta
matokeo chanya katika kuboresha hali ya usafiri majini ikiwemo Mamlaka
ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA, kwamba tulijifunza jambo
lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?
Na
Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo?.
Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhamana ya kusimamia
sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na
nchi kavu?. Je, tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji
pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu?.
Lakini
pia wapo waliohoji na bado wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti
ya uchunguzi wa ajali hiyo ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado wanaendelea kujiuliza, ni ajali ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo?
Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya watanzania wengine ikiwemo ile ya Mv.Spice Ireland iliyotokea Septemba 10, 2011 katika mkondo wa Nungwi Kaskazini Unguja Zanzibar.
Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya watanzania wengine ikiwemo ile ya Mv.Spice Ireland iliyotokea Septemba 10, 2011 katika mkondo wa Nungwi Kaskazini Unguja Zanzibar.
Lakini
yote tisa, kumi ni sintofahamu iliyoibuka juu ya chanzo halisi cha
ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa nchini. Wapo waliosema ilikuwa ni
uzembe wa wakaguzi na waangalizi wa vyombo vya majini kwa maana ya
mamlaka husika kama SUMATRA, wapo waliosema ilikuwa ni uzembe wa nahodha
na timu yake na wapo waliosema chombo kilikuwa kibovu.
Lakini
pia wapo waliodai chombo hicho kilikuwa kimebeba mizigo na abiria
kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe walisababisha
ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda melini ilihali chombo kilikuwa
kimejaa huku mrorongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali hiyo
na imani za kishirikina.
Sina
nia ya kuandika hayo yote kwa lengo la kumtafuta wa kumtishwa lawama,
laa hasha, ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo yote ili kila mmoja kwa
namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia ili kuhakikisha tunaeupakana
na na ajali za majini kumbuka wahenga walisema tusiangalie tulipoanguka
bali tuangalie tulipojikwaa.
Kumbuka
watanzania wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao na mmoja
wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha yake ni mwanamitindo
maarufu nchini, Flavian Matata ambaye alimpoteza mama mzazi pamoja na
binamu yake.
Pamoja
na watu wengine, Matata amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa
kufika jijini Mwanza katika eneo la Igoma ilipohifadhiwa miili ya
waliopeza maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba.
Yapo
mengi ya kuzungumza na kuandika lakini swali la kujiuliza ni moja tu,
miaka 21 mwaka huu 2017 tangu kuzama meli ya Mv.Bukoba mnamo Mei
21,1996, je usafiri wa majini nchini ni salama ama tunasafiri kwa kudra
za Mwenyezi Mungu?
Nihitimishe kwa kusema ni jukumu la kila mmoja kwa kushirikiana na mamlaka husika ikiwemo SUMATRA kuhakikisha kuwa usafiri wa majini unakuwa usafiri salama nchini.
Imeandaliwa na George Binagi @Binagi Media Group
Kwa msaada wa mitandao mbalimbali.
Nihitimishe kwa kusema ni jukumu la kila mmoja kwa kushirikiana na mamlaka husika ikiwemo SUMATRA kuhakikisha kuwa usafiri wa majini unakuwa usafiri salama nchini.
Imeandaliwa na George Binagi @Binagi Media Group
Kwa msaada wa mitandao mbalimbali.