http://www.malunde.com/2017/05/haya-ndiyo-maamuzi-magumu-ya-rais.html


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa mchanga unaosafirishwa nje kutoka kwenye baadhi ya migodi ya madini amezungumza mambo yafuatayo: 
1.Wapo waliotaka kuingilia uchunguzi huu na majina yao serikali inayo,wapo watu wamehongwa pesa na kuna wengine wamerekodiwa mpaka video!. 
2.Nchi ipo kwenye vita mbaya ya uchumi,makontena 3600 ya mchanga yenye madini yanasafirishwa kila mwaka kwenda nje!. 
3.Mali zinapotea,watanzania wamewekwa kusimamia na hawajali kuona mali zinaibiwa,ndiyo maana baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa wizara kutoa majibu ya uongo kwa wabunge,alifukuzwa papo hapo!. 
4.Watanzania katika vita hiii tuwe wamoja,wawekezaji hawa wamefukia hatua ya kuunder invoice kwenye kila jambo!. 
5.Kwenye eneo hili peke yake,nchi hii ilitakiwa kuwa inasaidia mataifa mengine na siyo kuwa omba omba!.Madini haya yanaaafirishwa bureee kwenda nje!. 
6.Viongozi wa wizara walikuwa wanakwamisha ununuaji wa smelter ili mchanga usafishiwe hapa nchini!. 
UAMUZI WA RAIS 
1.Mapendekezo yote ya kamati yamekubalika 
2.Bodi ya TMAA imevunjwa kuanzia leo. 
3.Chief executive wa TMAA anasimama na watumishi wote wa TMAA wachukuliwe hatua za kisheria!. 
4.Vyombo vya ulinzi na usalama vianze kutumika kwenye ulinzi wa mali za umma hususani zinazojusika na madini!. 
5.Vyombo vya ulinzi viwachunguze watendaji wa wote wa wizara ya nishati na madini!. 
6.Waziri wa nishati na madini aachie madaraka yake!
Mapendekezo ya kamati ni:
1. Isitishe usafirishaji wa mchanga mpaka mrabaha stahiki utakapolipwa serikali kwa kuzingatia thamani halisi ya makenikia.
2. Ujenzi wa *** unafanyika haraka ili makenikia hayo yasafirishwe ndani ya nchi ili madini yote yaweze kufahamika na kutozwa mrabaha sahihi.
3. Tepe za udhibiti zifungwe mara moja ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanyika wakati wa kuchukua sampuli.
4. TMAA ipime metali zote zilizomo kwenye makenikia ili kupata thamani halisi ya metali hizo (mrabaha).
5. Kutokana na kuwepo madini mbalimbali kwenye Mbale. TMAA ipime viwango vya metali zote muhimu ktk mbale zinazosafirishwa bila kujali kilichoandikwa kwa msafirishaji.
6.
7. Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wale wa wizara inayohusika.
8. Pamoja na vyombo vya uhakiki, serikali iweke mfumo wa kushtukiza ili kuepuka watendaji kufanya kazi kwa mazoea.
9. Serikali itumie wataalamu wa mionzi ili kufunga scanner zenye uwezo sahihi (kwa ajili ya makenikia na mizigo mingine).
Powered by Blogger.