https://binagimediagroup.blogspot.com/2017/05/timu-ya-azania-yawasili-nchini-baada-ya.html
Meneja
Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (nguo
nyeusi) akiwasili na Wachezaji wa Timu ya Azania katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea
nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road
to Anfield 2017.
Mashindano ya
kombe la Standard Chartered yaliyokuwa yanafanyika nchini Uingereza
yamemalizika na kombe hilo kutwaliwa na timu ya nchini Singapore.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuwasili timu ya
Azania iliyowakilsiha nchi za Afrika ya Mashariki, Meneja Uhusiano wa
Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga amesema timu ya
Azania ilikwenda Uingereza kushindana kwenye mashindano ya “Standard
Chartered-Road to Anfield” iliyokuwa inahusisha wateja wa benki hiyo.
Timu
zilizoshiriki kwenye mashindano hayo zilikuwa ni timu nane kutoka
Singapore, Uingereza, India, Nigeria, Botswana, Honk Kong, Korea na
Tanzania.
Katika
michuano hiyo timu ya Azania iliweza kutinga nusu fainali ambapo
ilicheza na Uingereza na kutolewa kwa mikwaju ya penati. Timu ya
Singapore iliibuka mabingwa wa kombe Standard Chartered –Road to Anfield
kwa mwaka 2017.
Mariam
alisema timu hiyo imefanya vizuri kwenye mashindano hayo japo
hawakufanikiwa kutwaa kombe hilo mara baada ya kutolewa kwenye michuano
hiyo.
Alisisitiza
wao kama Benki ya Standard Chartered Tanzania hawajakata tamaa na hii
ilikuwa ni fursa nzuri kwa vijana kuonesha vipaji vyao ili kufikia
malengo waliyojiwekea.
Na
pia ameipongeza timu ya Azania kuiwakilisha vyema Tanzania kwa kuwa ni
mara ya kwanza kuingia kwenye mashindano hayo na pia wamejitahidi
kupigana mpaka kufikia kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Nahodha
wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said ameishukuru benki ya Standard
Chartered Tanzania kwa kuona umuhimu wa michezo hapa nchini na wameweza
kujifunza mengi kwenye michuano hiyo iliyokuwa ikiendeshwa nchini
Uingereza ambapo timu yao ilitolewa kwenye nusu fainali. Lakini wao
wanaamini hapa ni mwanzo na watapigana mpaka siku kombe liweze kutua
hapa nchini. Wachezaji wa timu ya Azania wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Azania mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.
Wachezaji wa Timu ya Azania wakiwasiliana na ndugu jamaa na marafiki mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza.
Geofrey Adroph