HATUA ZA KUFUATA BAADA YA KUACHWA NA NDEGE.
Na Jumia Travel Tanzania
Ni
jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au ndege
licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu zinazoweza
kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni barabarani,
ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa kuwasili.
Hali ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana
kama haijawahi kukutokea kabla na hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha
kusafiri kama ulivyokukusudia.
Zipo hatua kadhaa za kufuata pindi
uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel ingependa uzifahamu na kuzizingatia
pindi utakapokumbwa na changamoto kama hii.
Wasiliana na shirika la ndege
unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kugundua kwamba
utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa kusafiri nayo ni
kuwasiliana na shirika husika.
Mara nyingi mawasiliano huwemo kwenye
tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni msaada gani
wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.
Kuwa makini na sheria na masharti ya
tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege linakuwa na taratibu za
uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo zinawasafirisha na ndege nyingine
wateja wao waliochelewa, zingine siku inayofuata kama hamna kwa siku
hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo
kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo au soma kwenye tiketi yako
kama zipo.
Usihamaki/usiwe na hofu. Wewe sio wa
kwanza kuachwa na ndege hali hiyo ishawakuta watu wengi hivyo vuta pumzi
na tuliza akili yako ili ujue nini cha kufanya.
Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya
tatizo haraka sana kama vile kuulizia cha kufanya, kuahirisha au
kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu ili usafiri na kuwahi shughuli zako
kama ulivyopanga. Kwani kama kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha
kufanya kutokana na hali hiyo.
Ulizia kwa wafanyakazi wa kampuni husika
ya ndege machaguo uliyonayo. Kama umeshindwa kupata mawasiliano au
haujui taratibu za shirika la ndege ulilokatia tiketi ya kusafiri basi
ni vema ukauliza.
Mashirika mengi yanakuwa na ofisi kwenye
viwanja vya ndege au kama hawana basi ulizia wafanyakazi wa pale
naamini wao wana uzoefu mkubwa wanaoweza kukupatia.
Lipia gharama za ziada baada ya kukosa
ndege kama ulishafika tayari. Kama unaona kwamba utachelewa shughuli
zako huko uendako basi huna budi kuongeza pesa kidogo ili uweze kusafiri
na ndege inayofuata.
Tazama kama kuna ndege zingine
zinazoelekea mahali uendapo. Kwa kawaida kwenye viwanja vya ndege vingi
kunakuwa na ubao unaoonyesha ndege za mashirika tofauti zinazokwenda
sehemu mbalimbali kwa siku hiyo. Hivyo inaweza kuwa fursa kwako kwa
kufanya maamuzi ya kukata tiketi ili kuwahi shughuli zako.
Tumia muda huo kufanya mambo mengine.
Kuchelewa safari haimaanisha kwamba ndiyo mwisho wa maisha. Kwa mfano
upo Arusha na umechelewa ndege ya kukurudisha Dar es Salaam kwa siku
hiyo, unaweza kuamua kutembelea vivutio kadhaa vilivyopo karibu na eneo
hilo kama vile hifadhi ya Serengeti au Ngorongoro au hata Mlima
Kilimanjaro.
Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema.
Mara nyingine huwa tunafikia kwenye hoteli kwa mahali tunapoelekea labda
uwe unarudi nyumbani.
Kwa hiyo nina uhakika utakuwa umelipia
hoteli wakuhifadhie chumba au kuomba usafiri wa kuja kukuchukua uwanja
wa ndege. Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema kwamba utachelewa au
utafika siku inayuofuata ili kuondoa usumbufu kwao na kulipishwa gharama
za ziada.
Jifunze kutokana na makosa yako. Kufanya
makosa ni sehemu ya kujifunza mambo mengi maisha yetu. Hivyo basi
hakikisha kwamba baada ya kuchelewa safari hii utakuwa makini zaidi
wakati mwingine.
Kama ulichelewa kwa sababu ya usafiri
basi hakikisha unatoka mapema zaidi, kama ni ulikosea kuangalia muda
basi muombe mtu wa karibu yako akukumbushe.
Sababu ni nyingi ni zingine haziwezei
kuzuilika kwa upande wa abiria na hata kwa shirika la ndege. Kuna wakati
mwingine unaweza kuchelewa ndege kutokana na sababu za kiufundi za
shirika lenyewe.
Mara nyingi kwa sababu kama hizo abiria
huwa wanafidiwa na mashirika ya ndege. Lakini kama ni sababu zako
binafsi, Jumia Travel inakuasa kwamba uwe makini kwani utaishia kupoteza
muda, kuvuruga mipango yako na kuingia gharama za ziada usizozitarajia.