DIWANI WA KATA YA BUZURUGA JIJINI MWANZA AONGOZA WAKAZI WA KATA HIYO KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI KATIKA KITUO CHA AFYA BUZURUGA.
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya
Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machema (kushoto), akishiriki zoezi la
usafi pamoja na Wananzengo wengine wa Kata hiyo katika Kituo cha Afya
Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani, Mei Mosi, 2017.
BMGHabari
Wananzengo wa Kata ya Buzuruga wakiwa
pamoja na diwani wao, Richard Machema (mwenye kofia), katika zoezi la
usafi kwenye Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
Zoezi la usafi la kuondoa vichaka na
taka katika mazingira ya Kituo cha Afya Buzuruga limeelezwa kusaidia
kuteketeza maficho ya masalia ya mbu pamoja na baadhi ya vijana wasio na
maadili mema waliokuwa na desturi ya kujificha kwenye vichaka hivyo kwa
sababu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa bangi.
Uteketezaji wa taka hatarishi ikiwemo
chupa umelalamikiwa na wakazi wa Kata ya Buzuruga na kuomba suala hilo
kufanyiwa kazi ili kuwa na uteketezaji taka usio hatarishi katika jamii
Usafi ukiendelea
Usafi ukiendelea
Mwananzengo wakiongea na Lake Fm kuhusiana na usafi huo
George Binagi-GB Pazzo
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo, Machemba amesema uamuzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya
kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani hii leo na kwamba hatua
hiyo pia itasaidia kuondoa hatari za kimazingira ikiwemo magonjwa kituoni hapo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Afya Kituo cha Afya Buzuruga, Daniel Buluya, amesema awali
mazingira ya Kituo hicho hayakuwa salama hatua ambayo ilikuwa inahatarisha
usalama wa wagonjwa na watumishi wa afya kituoni hapo.