BABA AMKATA MAKALIO MTOTO WAKE HUKO MWANZA
Mwanamume mmoja mkazi wa Ndofe wilayani Nyamagana mkoani Mwanza
amemfanyia kitendo cha ukatili mtoto wake kwa kumkata na kisu sehemu za
makalio kwa madai ya utoro shuleni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa
huyo kuwa ni Nuhu James (50) anayedaiwa kumfanyia ukatili mtoto Ndalo
Nuhu (14) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari
Igoma kwa kumfunga kamba miguuni na mikononi kisha kumchapa fimbo sehemu
mbalimbali za mwili wake na baadaye kumkata na kisu sehemu za makalio,
tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 11:00 alfajiri ya tarehe 25
Mei, 2017.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliaamua kumfanyia ukatili wa aina hiyo mtoto wake baada ya kugundua kwamba mwanaye ni mtoro shuleni.
Kamanda Msangi amesema baada ya mama wa mtoto alipoona ukatili
anaofanyiwa mwanaye na hali yake kiafya kuzidi kubadilika alishindwa
kuvumilia na arehe 28 Mei.2017 aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi
Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa polisi wapo katika upelelezi na
mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani huku majeruhi akipelekwa hospitali kwa ajili ya
matibabu na hali yake inaendelea vizuri.