YANGA YATAKA WALIOCHANGIA SIMBA KUPEWA POINTI TATU WAFUKUZWE KABISA KABISA
Yanga imetangaza kutokuwa na imani tena na watendaji na wafanyakazi wote ndani ya bodi ya Ligi.
Hilo limetangazwa na uongozi wa Yanga kupitia mjumbe wa kamati ya klabu hiyo, Salum Mkemi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo, Mkemi amesema wafanyakazi wa bodi hiyo wanapaswa kufukuzwa.
“Waamuzi
wameondolewa kutokana na tuhuma, tumeshangazwa na mashaka na hatuna
imani na watendaji wa bodi ya ligi, hadi mtendaji mkuu.
“Vipi
wanashindwa kuwa na kumbukumbu, eti walienda kumuita mwamuzi atoe
ufafanuzi. Je, angekuwa mgonjwa au alishafariki? Kuwapa Simba pointi
tatu, inaonyesha wanapaswa kuwajibishwa na kufukuzwa mara moja,” alisema
Mkemi akionekana ana jazba.