YANGA YAMUACHA CHIRWA SAFARI YA ALGERIA, BARTHEZ, ZULIU NAO WABAKI





Yanga inaondoka kesho saa 12 jioni kwenda Algeria ikipitia Dubai.

Yanga inakwenda kucheza mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya MC Alger ambayo ilikubali kipigo cha bao 1-0 jijini Dar.

Kitakuwa kikosi cha watu 20 bila ya mshambuliaji hatari Obrey Chirwa ambaye imeelezwa ana matatizo ya kifamilia.


Wachezaji wengi wanaokosa mechi hiyo ni Ally Mustapha 'Barthez', Pato Ngonyani, Justine Zulu, Yusuf Mhilu na Anthony Matheo.

TAARIFA YA YANGA KUHUSIANA NA KIKOSI KIZIMA KINACHOKWENDA ALGERIA, HII HAPA.


Powered by Blogger.